GET /api/v0.1/hansard/entries/806083/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 806083,
    "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/806083/?format=api",
    "text_counter": 146,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante Bw. Naibu Spika. Ninafuraha ukiwa kwenye kiti kwa sababu utanipa nafasi nyingine. Kama vile Waziri Matiang’I alisema, sukari haramu ina mercury. Nimeona watu kutoka Kaunti moja ya Kisii wakisema wameletewa sukari bali hii sio sukari peke yake. Sukari hii ilingia katika Port ya Mombasa na imeuzwa Busia na kila mahali. Inawezwa kuwa iko Kilifi pia. Kwa nini wanabiashara kama wale wanaharibu maisha ya Wakenya wote bila kujali kwa sababu wanapata pesa kupitia uuzaji wa sukari ambayo wameleta kwa njia ya nyuma? Mahakama inafaa iwachukuliwe hatua wale wote wanashtakiwa kwa makosa kama hayo. Tunataka Waziri Matiang’I afanye bidii ili watu hawa washikwe na wapelekwe kortini, wachukuliwe mkondo wa sheria na hatimaye wafungwe."
}