GET /api/v0.1/hansard/entries/806108/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 806108,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/806108/?format=api",
"text_counter": 171,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii. Ni jambo la kusikitisha sana katika Jamhuri yetu ya Kenya, hususan wakati huu ambapo watu wamefanya ‘handshake’ na kuna uwiano mwema ya kwamba kuwe na amani na uchumi wetu upande juu ili watu wapate manufaa ya maisha bora. Bw. Naibu Spika, kitu cha kwanza ni kumshika Mkenya mwenye kosa na kumweka ndani ya korokoro aidha akiwa ni askari au raia. Wakenya wote ama watu wa nchi yoyote tunajua kwamba lazima sheria ifuate mkondo wake. Kwanza nataka kuwapaa kongole maafisa wa jeshi waliokuwa wakitetea nchi yetu na tumeona kuwa wengi wao wamekufa wakiitetea nchi yetu ya Kenya. Ni jambo la aibu hivi sasa kukumbuka yaliyotendeka wakati huo. Wanajeshi walishikwa, wakatupwa ndani ya korokoro na wakateswa zaidi. Hatimaye walipotolewa, wakafutwa kazi. Sasa, utapata kwamba mtu anaadhibiwa mara mbili; kwanza anatolewa jeshini na kuwekwa ndani. Kitu cha pili, anapoteza kazi yake. Bw. Naibu Spika, ni jambo la kusikitisha kwa mtu kupoteza kazi yake, kwa sababu ni kukaribisha umaskini ndani ya nyumba. Vile vile, ni jambo la kisikitisha kwamba baada yao kwenda kortini kutafuta haki zao, tumeona kwamba haki haitendwi na Serikali. Wamepata orders kortini iliyoamrisha Serikali iwajibike na kuwalipa. Hata The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}