GET /api/v0.1/hansard/entries/806110/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 806110,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/806110/?format=api",
"text_counter": 173,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kama Serikali haikubaliani na uamuzi wa korti, wanafaa kulipa kwanza, halafu watafute nafasi ya kukata rufaa baadaye. Lakini tunaona Serikali imelegeza miguu, mikono na mwili mzima na kukataa kutii amri ya korti. Ikiwa Serikali itakataa kutii amri ya korti, basi tunasema kuwa hakuna Serikali katika ulimwengu itakayo weza kuendesha Serikali yake ama baadhi ya vitu ambavyo inatakikana kuwafanyia wananchi wake iwapo haitatii amri ya korti. Bw. Naibu Spika, ni jambo la kisikitisha tukiona kwamba hivi sasa wameenda kortini, wakapata orders kuamrisha walipwe zile pesa, ambazo ni haki yao. Lakini mpaka sasa, hilo halijafanyika hadi wengine wamekuwa wazee, mababu na hata vikongwe. Niko na hakika kwamba hata wengine walikufa. Pengine pesa hizi zingeenda kwa jamii zao ziwasaidie. Bw. Naibu Spika, ni jukumu la Serikali kutii order ya korti. Ikiwa Petition kama hii itakuja---"
}