GET /api/v0.1/hansard/entries/806475/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 806475,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/806475/?format=api",
"text_counter": 215,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa ambayo imetolewa na ndugu yetu Seneta. Ni kweli kuwa sukari nyingi inayoletwa katika nchi ya Kenya inapitia katika bandari ya Mombasa. Ni kweli pia, kuwa mara ya mwisho sukari ililetwa na kuwekwa kwenye mabohari ambayo yako wazi na hutumika kwa kuweka clinker ambayo inatumika kutengeneza simiti. Hatari iliyoko ni kwamba Wakenya wengi ambao wametumia sukari hiyo wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa Saratani kutokana na madini mabaya ambayo yako katika kemikali ya clinker ambayo inatumika kutengeneza simiti. Katika eneo la Owino-Uhuru Mombasa, nyumba nyingi na wakazi wameathirika kwa sababu ya vumbi inayotokana na ile clinker inayowekwa hapo ili kutengeneza simiti. Kuna shirika ambalo linaitwa Kenya Plant Health Inspectorate Service (KEPHIS) ambalo linahusika na kukagua vyakula vinavyo ingia katika nchi ya Kenya na vinavyo pelekwa nje ya Kenya. KEPHIS ina ofisi katika sehemu ambapo bidhaa zinaingilia na kutoka katika nchi ya Kenya. Ninashangaa kuona kwamba KEPHIS inaweza kuruhusu sukari ambayo inamadini ambayo yanadhuru binadamu kutumika katika nchi ya Kenya. Bw. Naibu Spika, tumeona mara kwa mara Serikali ya Kenya ikiomba kuongezewa muda ili kutekeleza maazimio ya COMESA kuhusiana na sukari inayoletwa katika nchi ya Kenya. Mpaka sasa, mbali na kwamba viwanda vinaendelea kufilisika, sukari bado inaletwa kutoka nchi zingine kama vile Brazil, ambayo ni kinyume na kanuni za nchi na Serikali inapoteza ushuru mkubwa kutokana na sukari hiyo ambayo inaingia katika nchi ya Kenya. Hii ina maana kuwa tutaendelea kuagiza sukari kutoka nchi za nje The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}