Asha Hussein Mohamed

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1 to 10 of 13.

  • 17 Nov 2021 in National Assembly: Asante sana, Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Mswada huu wa kusajili makundi ya jamii. Tuna makundi tofauti tofauti katika jamii zetu, haswa katika Kaunti ya Mombasa. Tuna makundi yaliosajiliwa lakini hayana uwezo wa kuendeleza shughuli zao na yanapopata pesa za Serikali huwa yanazifuja vibaya. Kwa hivyo, naunga mkono usajili huu kwa sababu makundi hayo yatakuwa yanafuatiliwa ili yaweze kujiendeleza yenyewe kiuchumi, yaendeleze miradi yao mbali mbali na kujimudu kimaisha. Kwa hivyo, naunga mkono haya makundi kwa sababu tunapoelekea, tunataka makundi hayo yapewe pesa nyingi zaidi kwa sababu ya ubunifu wa kufanya miradi. Yanaweza kuvumbua miradi mipya tofauti ili ... view
  • 6 May 2021 in National Assembly: Hon. Speaker, I vote Yes for the BBI. view
  • 6 May 2021 in National Assembly: Yes, Hon. Speaker. view
  • 11 Mar 2021 in National Assembly: (Mombasa (CWR), ODM): Thank you, Hon. Deputy Speaker. I wish to ask the Cabinet Secretary for Agriculture, Livestock and Fisheries whether he could explain the measures the Ministry is putting in place to secure local and international markets for coconut, which has been categorised as a scheduled crop in the Crops Act, 2013? view
  • 11 Mar 2021 in National Assembly: Thank you. view
  • 21 Nov 2019 in National Assembly: Thank you, Hon. Speaker. My Question goes to the CS for Education: (i) How many school leavers are yet to receive their school certificates from their former learning institutions due to fees balances in Mombasa County? (ii) Could the Cabinet Secretary state the action taken against secondary schools that are yet to release Kenya Certificate of Secondary Education (KCSE) certificates to all former students in Mombasa County in compliance with the Government directive of July 2014? view
  • 8 Aug 2018 in National Assembly: Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwanza, naunga mkono Mhe. Jessica Mbalu kwa kuleta Hoja hii. Naiunga mkono kwa sababu itakuwa vyema Serikali itakapoweza kutenga pesa hizi kujenga vituo hivi vya ushauri dhidi ya ubakaji na dhuluma za kijinsia. Tunaona watoto wetu wakiteseka sana katika jamii. Wanapopata matatizo, kudhulumiwa na kurudi nyumbani, wengine huenda wakarukwa na akili. Kuna wale wamerukwa na akili kwa sababu ya ubakaji na hivyo, kupoteza hamu ya kuishi katika jamii. Serikali itakapotenga pesa hizi na vituo hivi kujengwa ili hao watoto wetu na akina mama wanaodhulumiwa waweze kupata ushauri na kuondoa unyanyapaa katika jamii, itakuwa ... view
  • 18 Apr 2018 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu wa Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Kwanza, nampongeza Mhe. Martha Wangari kwa Hoja hii. Hili limekuwa kama janga Mombasa na Kenya nzima. view
  • 18 Apr 2018 in National Assembly: Kwa sababu ya umaskini, kuna wazazi wengine hawana pesa ya kulipa stakabadhi ya kuzaliwa kwa watoto wao. Wanapozaa ndani ya nyumba, hawaendi kuandikisha watoto wao. Kuna wazazi wengine ambao wanapeleka watoto kliniki. Baada ya muda wa miezi tisa ama mwaka mzima wanamaliza kliniki, kulingana na yale makaazi nyumbani, wale wazazi wanapoteza zile kadi za kliniki. Unapokwenda kujiandikisha, ni lazima uwe na stakabadhi ya kuzaliwa kwa mtoto na kadi ya hospitali ya chanjo. Kuna ndoa za mapema: Utakuta mtoto anazaa mtoto. Wakati wakuchukuwa hii stakabadhi, inagundulika kwamba mama hana kitambulisho ambacho kinahitajika ili kusajili mtoto aliyezaliwa. Kunao wajane na wale single ... view
  • 18 Apr 2018 in National Assembly: TungependaWakenya wapate stakabadhi hizi kwa urahisi katika vituo vya usajili. Hapo awali wakati nikienda shule mwaka wa1983 nilishika sikio nikaingizwa darasani. Kwa hivyo Serikali yetu ichukulie maanani suala hili ili vyeti hivi vipeanwe kwa urahisi ili wazazi wasitaabike. Nakumbuka wakati nilipomaliza kidato cha nne nilipatiwa kitambulisho changu cha kitaifa shuleni huko Giriamani, Kadzonzo Girls. Wasajili walikuja shuleni wakasema wale ambao wamefikisha miaka 18 wajiandikishe. Tulipatiwa vitambulisho vya kitaifa katika shule na tunazitumia hadi leo. Sioni ni kwanini iwe vigumu wazazi kupata huduma hii. Ombi la Mheshimiwa litiliwe maanani ili wapate stakabadhi hizo. The electronic version of the Official Hansard Report ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus