Kalembe Ndile

Full name

Kalembe Richard Ndile

Born

16th April 1964

Post

P.O. Box 255 Kibwezi, Kenya

Telephone

0722 352009

All parliamentary appearances

Entries 11 to 20 of 28.

  • 29 May 2007 in National Assembly: You are misleading us! view
  • 29 May 2007 in National Assembly: Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Isipokuwa sijaona jina la Mkamba hapa, najua Kenya--- view
  • 29 May 2007 in National Assembly: Wewe na wewe! view
  • 29 May 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, ninasema kwamba hata kama sijaona jina la Mkamba hapa, naamini Kenya ni kubwa na tuko na makabila mengi sana. Kuna msemo mmoja wa Kiswahili unaosema kwamba: "Kinyozi hajinyoi." Yale matatizo ambayo tuko nayo hapa Bungeni, ambapo watu wanasema kwamba hawakuwekewa majina waliotarajia, ni wao walitaka kujinyoa kwa sababu tulianza na wao na wakadanganyana, wakasema kwamba huu ni mchezo wa mpira. Walifikira kwamba siasa ni mchezo wa mpira. Ningependa kusema kwamba hakuna jina la Mkamba katika orodha hii, kwa sababu mtu mmoja aliwadanganya Wakamba wetu na wakaenda upande ule. Wangekuwa upande huu, tungekuwa na jina moja ... view
  • 29 May 2007 in National Assembly: Jambo la nidhamu, Bw. Naibu Spika wa Muda. Je, ni nidhamu kwa Maj. Madoka kuipotosha Nyumba hii kwamba kilo moja ya mahindi imepanda bei hadi Kshs100 na ilikuwa Kshs50 zamani, akijua kwamba wakati huo, walikuwa wakinunua gunia ya mahindi kwa Kshs300 na sasa iko Kshs1200. Hiyo ni kutupotosha! view
  • 9 May 2007 in National Assembly: On a point of order, Mr. Temporary Deputy Speaker, Sir. view
  • 9 May 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, ni haki kwa Bw. Ntimama kudai kwamba uchumi wa nchi hii bado haujakua, na hali tunafahamu kwamba alipokuwa Waziri katika Serikali iliyopita, alichangia kuanguka kwa uchumi kwa kuwaambia watu kutoka jamii fulani walale chini kama bahasha? view
  • 27 Mar 2007 in National Assembly: Ahsante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Kabla sijaongea juu ya Hotuba ya Rais, ningependa kuchukua nafasi hii kukushukuru kwanza kwa kutambua kwamba Wabunge wanafanya kazi. Kuna watu wengine ambao wanafikiria tulichaguliwa kufanaya kazi hapa Bungeni peke yake. Hawajui kwamba tunafanya kazi nyingi sana huko nje. Lakini uliwakumbusha. Bw. Spika, Hotuba ya Rais ilikuwa na mambo mengi sana. Ningependa kusema kwamba labda mimi sielewi sheria. Bado ninajifunza. Lakini, nakumbuka kuna sheria ambayo tulipitisha hapa Bungeni! Tulisema kwamba zawadi kwa Wabunge inayopita Kshs10,000 ikabidhiwe kwa Bw. Spika. Wakati niliona gari lingine hapa nje, nilifikiri ni lako kwa sababu ni zawadi ... view
  • 27 Mar 2007 in National Assembly: Bw. Spika, sijui ikiwa nilielewa vibaya, lakini nilisikia kwamba hilo gari linaloitwa "nyundo" ni zawadi. Nakumbuka Wakenya walioko ng'ambo walipiga kelele sana wakati Wabunge walinunuliwa magari na Serikali. Walisema Wabunge walipewa magari ya bure. Wakati wa ukame, nilitoa gari langu liuzwe lisaidie watu wangu. Watu wanaongea juu ya ufisadi Serikalini lakini hapa nje, kuna mambo mengi sana ya ufisadi. Tunaiomba Serikali iangalie mambo hayo. Wakati huo wa ukame huo, Rais alitangaza kuna janga la njaa hapa Kenya. Kulikuwa na picha mbaya za watu walioathiriwa na baa la njaa. Kule kwangu, watu walikufa kwa kula mahindi yenye aflotoxin. Lakini, kuna mtu ... view
  • 27 Mar 2007 in National Assembly: Bw. Spika, nasema hivyo kwa sababu hapa kuna siasa za kujificha na kuwadang'anya Wakenya. Ni lazima sisi viongozi tuanze kuaminiana. Kwa mfano, kuhusu mambo ya uraia, nina dadangu ambaye ameolewa ng'ambo. Ikiwa yeye amekuwa raia huko, hawezi kuja huku kwa sababu yeye ni raia wa kule na hawezi kupata uraia wa hapa lakini ni dadangu. Hakuna mtu alikataa hilo jambo. Lakini hawa walisema kuwa eti sheria haisemi hivi, inasema kuwa wanawake watatahiriwa! Siamini kuwa hata sasa tukisema tunataka kubadilisha Katiba, ni nini itawekwa kwa vichwa vyao waseme ukweli. Ikiwa hawatasema ukweli, labda wengine watasema ukweli. Sisemi ni upande fulani, lakini ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus