All parliamentary appearances

Entries 11 to 20 of 262.

  • 15 Feb 2017 in National Assembly: powers to conduct impromptu visits to these facilities to be sure that there is a proper environment and infrastructure for training. We also realise that the Council, under Clause 5, is also empowered to ensure that there is a minimum entry in terms of academic requirements. This is very important because we really want to see a situation where graduates enter the profession at more or less an equal level. We do not want to see a situation where one gets a D+ and another gets a C+ and still find himself or herself in the same profession. This will ... view
  • 14 Feb 2017 in National Assembly: I support. view
  • 14 Feb 2017 in National Assembly: I agree, Hon. Temporary Deputy Chairman. I support this amendment. I think the idea here is to have some mechanism in which the county governor or the nominating authority will really get the people who will add value to the affairs that are supposed to be discharged. So, I support. view
  • 14 Feb 2017 in National Assembly: Yes, Hon. Temporary Deputy Chairlady. I wish to support the amendments, in particular the one that deletes the requirement for a medical certificate evidencing soundness of mind. I find that not necessary. view
  • 1 Feb 2017 in National Assembly: Shukrani sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa niungane mkono na wenzangu kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa hapa na Mhe. Njomo. Hoja hii inazungumzia ushawishi katika masuala ya uandikishaji wa kura. Ukipata fursa ya kuisoma, utaona kwamba leo inazungumza kuhusu kushawishi watu kuchukua kura na baadaye pia waweze kuhusika katika uchaguzi mkuu bila shaka hapo Agosti mwaka huu. view
  • 1 Feb 2017 in National Assembly: Jinsi tunavyojadili Hoja hii, ni lazima tuiangalie mara mbili. Kwanza kwa sasa vile tutazungumza na watu mpaka wachukue kura na bila shaka baadaye njia gani zitatumika ili waweze kuhusika katika uchaguzi mkuu. Ninasema haya kwa sababu nimeona sana wengi wa Waheshimiwa wakizungumza tu juu ya suala la kushawishi watu kuchukua kura. Baadaye ni lazima washawishiwe jinsi gani watakaoweza kupiga kura. view
  • 1 Feb 2017 in National Assembly: Kura kuweza kupigwa ni lazima kuwe na vitambulisho. Na inahuzunisha kwamba mara nyingi katika Jamhuri yetu ya Kenya, utoaji na usajili wa vitambulisho umekuwa duni sana. Ni juzi tu Mhe. Rais aliona atafute mbinu ambayo inaweza kufanya jambo hili lifanyike kwa haraka. Ni vyema lakini ilikuwa imechelewa. Kwa hivyo, ningependa kutoa mwito kwamba suala la uandikishaji wa vitambulisho liwe linafanywa kila wakati na suala linafanywa bila kuwa na gharama yoyote. Watu wetu wengi hawajachukua vitambulisho hivi kwa sababu mahali vinachukuliwa ni mbali na ni gharama kupata stakabadhi hizi. view
  • 1 Feb 2017 in National Assembly: Baadhi ya vitambulisho hivi pia vimekuwa vikifika katika vituo, kwa machifu na mahali kwingine vikiwa na makosa fulani fulani. Ningependa kusema ya kwamba wale ambao wanasajili vitambulisho hivi ni muhimi wawe waangalifu ndio tusiweze kuwa na majina ambayo hayaeleweki wakati watu wanapopewa vitambulisho hivi. view
  • 1 Feb 2017 in National Assembly: Siasa ama upigaji kura ni ushawishi. Kwa hivyo, ikiwa Hoja itazungumza kuhusu kuwashawishi watu wachukue kura, tunaelekea sawa. Kwa sababu hiyo, ni lazima tukubali kwamba jukumu la kushawishi watu wachukue kura ni letu kama wanasiasa hasa Wabunge na ni jukumu la vyama vya kisiasa. Ndio maana mimi nikiwa naongoza chama changu cha KADU- Asili, nimekuwa mstari wa mbele kuzungumza na watu kwamba ni muhimu kuchukua kura. Nataka nichukue fursa hii hapa katika Bunge hili la kitaifa niseme kuwa kuna umuhimu watu wachukue kura hususan watu wetu kutoka Mkoa wa Pwani na Kaunti yetu ya Kilifi ndio wafanye uamuzi wa busara. view
  • 1 Feb 2017 in National Assembly: Kumekuwa na changamoto nyingi sana katika masuala haya ya kuchukua kura. Kaunti yetu ya Kilifi, kwa mfano, imegonga vichwa vya habari kwa suala la baa la njaa. Suala hili la ukosefu wa lishe limechangia kwa kiasi kikubwa watu kutochukua kura katika Kaunti yetu ya Kilifi. Nataka nizungumze tu bila wasiwasi kuwa Serikali iko na jukumu la kuja na mbinu ya kuhakikisha kwamba watu wanaweza kupata lishe. Wakipata lishe, wataweza kuhusika katika hali kubwa ya kuweza kuchukua kura hizi. Haimaanishi watakapopewa lishe ndio lazima watapigia kura mrengo fulani. Hayo yatakuwa masuala ya baadaye. Kwa hivyo, saa hii ni kuhakikisha kwamba mbinu ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus