25 Jul 2018 in National Assembly:
(Lamu CWR, JP)
view
4 Jul 2018 in National Assembly:
Asante, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia hii nafasi ya kuchangia. Naona huu ni Mswada mzuri ambao utasaidia sana. Pia, nakubaliana na Wabunge waliotangulia kuchangia kwamba kuna matatizo. Watu wengine wanakataa fidia ya shamba ambayo wanapewa na Serikali na wanasiasa wanaingilia. Kuna sehemu zingine ambazo ziko na matatizo zaidi. Watu wengine wanasema wamelipwa fidia kidogo ama wanataka Wabunge waingilie ili waseme walipwe vizuri. Sehemu zingine kuna matatizo, kwa mfano Lamu East. Kuna sehemu katika Kisiwa cha Pate ambazo hata Mhe. akienda anaona ni sawa. Mtu anaambiwa mnazi ukatwe alipwe Kshs3,000 na ataona ni dhuluma ya wazi. Utaona barabara ilikuwa gazetted ...
view
4 Jul 2018 in National Assembly:
Huu Mswada utasaidia katika Kaunti ya Lamu kwa sababu fidia itawekwa usawa. Katika sehemu zingine, gogo la stima linapita na watu wanalipwa Ksh500,000. Kisha mtu mwingine kwa hiyo Kaunti, analipwa Kshs3,000 na pengine umegawanya shamba lake. Limekuwa nusu na hawezi kuweka fence vizuri kwa sababu barabara imepita. Huu Mswada ukifuatwa vizuri utatusaidia sana. Utaleta usawa. Mara nyingine utaona majina yameandikwa na hayajulikani ni kina nani kwa sababu yamefichwa. Hawaweki uwazi. Unashangaa kwa nini haya majina hayawekwi wazi. Kuna tatizo gani. Huu Mswada unazungumzia mambo ya Internally Displaced Persons (IDPs). Itakuwa ni vizuri katika Kenya nzima tujue kwamba kuna sehemu zingine ...
view
4 Jul 2018 in National Assembly:
Ukiyasema haya mambo ya ardhi, watu huinua macho mpaka unaonekana saa nyingine wewe ni mbaya. Kuna ile cartel ambayo inangojea utaje mambo ya shamba. Mhe. Ruweida akizungumza mambo ya ardhi leo, watu wengine watatuma ujumbe waseme miaka mitano. Hii ni kwa sababu mtu amepata asilimia 10 na anasema unapinga mradi na kuchochea wananchi lakini unawatetea. Sisi tumeletwa hapa kutetea watu. Ukiitwa uende, wengine wanasema unapinga mradi. Watu wanataka miradi lakini usawa ufanyike.
view
4 Jul 2018 in National Assembly:
Mhe. Spika wa Muda, sina mengi zaidi ya hayo. Asante.
view
27 Jun 2018 in National Assembly:
Asante, Mhe. Naibu Spika. Lamu Kaunti imeathirika pakubwa na haya matatizo. Jambo hili limeleta shida sana. Kuna watu ambao nyumba zao zimevunjwa na maji. Kuna mama ambaye alitoka Chalaluma kuenda kujifungua hospitalini Witu, lakini kwa sababu ya kupanda kidau cha mbao kwa sababu pale Chalaluma kulikuwa kumezingirwa na maji, alijifungua ndani na mtoto akafariki. Kuna matatizo mengi Lamu Kaunti. Wenyeji ni maskini na kumetokea magonjwa mengi kama vile malaria. Tumepata msaada wa chakula lakini shida bado ni nyingi. Kuna wanyama ambao wamepotea. Mamba wanatembea na hata sisi wenyewe imebidi tuingie katika hiyo maji na mamba wako tele.
view
27 Jun 2018 in National Assembly:
Haijatosha. Lamu imeathirika pakubwa na ni muhimu kamati husika iangalie mambo haya na hatua ya haraka ichukuliwe.
view
27 Jun 2018 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono Hoja hii. Inafaa tujue kaunti ambazo hazijachukua vijana NYS ama mara nyingine wanachukua vijana wachache sana. Sina mengine ya kuzungumza kwa sababu nangojea Hoja ingine ya Cashew Nut. Ni muhimu wakumbuke zile kaunti ambazo ziko marginalised . NYS inafaa kuchukua vijana wengi si kutupatia nafasi ya watu watatu ama wanne. Hata sisi tunataka nafasi zakutosha. Asante. Mhe. Naibu Spika wa Muda.
view
21 Jun 2018 in National Assembly:
Thank you, Hon. Speaker. Hon. Speaker, pursuant to Standing Order No. 43, I wish to make a Statement regarding the challenges currently facing the Kenya Wildlife Service. Hon. Speaker, the socio-economic importance of the wildlife sector remains central to the economic sustainability of our country. For instance, besides being a major foreign exchange earner through various products, the wildlife sector, contributes to the positive growth of the hotel industry, curio, transport industry and other inter-linking private service sectors thereby acting as a direct source of employment opportunities for thousands of Kenyans. It is worrying that despite the many benefits we ...
view