Sara Paulata Korere

Parties & Coalitions

Telephone

0727027937

All parliamentary appearances

Entries 11 to 20 of 351.

  • 22 Mar 2023 in National Assembly: When you refuse to win elections, please, deal with your matter. If you know that for you to win elections in Kenya you must steal, you should have invested in stealing! view
  • 22 Mar 2023 in National Assembly: Relax, hold your horses, Members. As a mother, my heart goes out to the woman whose son was killed in Maseno. It should not have happened, and should never happen. However, if demonstrations have to continue on Monday, we have to propose a few things that we have to list down so that we also think whether we can join those demonstrations. Hon. Temporary Speaker, you said that we should not name people in this House who cannot defend themselves. I am a Jubilee Party Member and my party leader is the de facto, Uhuru Muigai Kenyatta There were demonstrations ... view
  • 15 Mar 2023 in National Assembly: Shukrani Spika wa Muda. Kwanza, ningependa kumpongeza Mhe. Mohammed Ali ambaye amewasilisha Hoja hii. Baada ya yeye na mwenzake kuiafiki Hoja kwa lugha sanifu ya Kiswahili, sina budi bali kujikakamua kuzungumza Kiswahili changu chote cha bara, mradi tu niwasilishe yale ninayo. Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni. Masuala ambayo tunajadili leo katika Ukumbi huu tungeyajadili miaka iliyopita, ingekuwa ni mwiko. Hii ni maana kuzungumzia hayo masuala kwa mila na tamadhuni zetu, haingekuwa jambo la kawaida. Lakini, imebidi tuyajadili maana ni mambo ambayo yamekuwa yakisambaa. Kwa lugha ya kisasa itasemwa kwamba yamesambaa ‘chini ya maji’. Leo hii yamejitokeza wazi na kwa ... view
  • 15 Mar 2023 in National Assembly: mwilini; na tundu lingine lipo la kuondoa uchafu mwilini ambalo wengine wanataka kugeuza liwe la kazi nyingine. Hayo, ni makubwa sana. Lakini cha kutisha mno ni kwamba wakoloni walikuja kwetu na wakatuonyesha kuwa kila kitu ambacho kinaambatana na mila zetu ni kibaya. Pia, kila kitu cheusi ni kibaya. Wametengeneza na kutuletea filamu zao zinazomwonyesha shetani kuwa na rangi nyeusi. Labda shetani alikuwa mweupe pe pe pe, hatujui! Tulitiwa kasumba ya kuchukia kila kitu chetu ambacho ni kizuri na kununua yale ambayo ni mabaya. Sasa, wamechukua hatua nyingine kwamba sharti ufanye hili ama lile ndiyo watoe misaada fulani. Mimi nataka kuwaambia ... view
  • 23 Feb 2023 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wa Muda naomba nikushukuru. Wahenga wanasema mficha uchi hazai. view
  • 23 Feb 2023 in National Assembly: Kinara wa Waliyo Wachache Bungeni alipozungumza alisema kwa kimombo kwamba wanataka kuchukua hatua za kinidhamu. Utasikiza alivyosema. Mhe. Junet aliposema kuwa wale wanataka kuenda kuchukua nafasi zao katika Kenya Kwanza waende, ninamjulisha kuwa hatuendi. Iwapo wana njia yakutupeleka watafute tingatinga watupeleke. Tutakaa kwenye huu mrengo. Ndugu yetu ambaye ni Kinara wa Wachache hana ule uvumilivu wa kusikiza mawaidha yanayotofautiana na yake. Kwa Kiingereza inaitwa intolerance. Kila mmoja aliye kwenye jumba hili alichaguliwa na alitumia mali zake, akili na hata muda wake kutafuta kura, kujitafutia na kutafutia mrengo wake wa kisiasa. Tusifike hapa watu waanze kuhujumu wenzao kwa sababu wengine wetu ... view
  • 23 Feb 2023 in National Assembly: mbaya zaidi kuliko ile imla tuliyoshuhudia katika hii nchi miaka iliyopita. Hatuwezi kuomba mtu ruhusa ya kuenda ikulu. view
  • 23 Feb 2023 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wa Muda naomba nikushukuru. Wahenga wanasema mficha uchi hazai. view
  • 23 Feb 2023 in National Assembly: Mheshimiwa Spika ninavyoelewa mimi ni kwamba, kila Mheshimiwa katika Jumba hili ana wajibu wa kuhakikisha kuwa serikali imewajibika. Awe wa upande ule ama upande huu. Ninashangaa kizaazaa ambacho ndugu yetu Kinara wa Waliowachache anataka kuleta kisiri ni cha nini. Iwapo kizaazaa kipo, wasifanye kisiri bali walete kinaga ubaga kwa kuwa chama ninachosimamia… Wajua waswahili husema paka akiondoka panya hutawala. Mhe. Uhuru alipoondoka Jubilee kwa sasa mimi ndiyo Kinara wa chama wa muda. Iwapo wana ODM wanataka mazungumzo basi wazungumze nami. Naomba Kiongozi wa Waliowengi Bungeni alinde uhuru na haki za Wabunge. Ashirikiane na ndugu zetu kwenye Bunge. Waache kwenda Jeevanjee. ... view
  • 23 Feb 2023 in National Assembly: Kinara wa Waliowachache Bungeni alipozungumza alisema kwa kimombo kwamba wanataka kuchukua hatua za kinidhamu. Utasikiza alivyosema. Mhe. Junet aliposema kuwa wale wanataka kuenda kuchukua nafasi zao katika Kenya Kwanza waende, ninamjulisha kuwa hatuendi. Iwapo wana njia yakutupeleka watafute tingatinga watupeleke. Tutakaa kwenye huu mrengo. Ndugu yetu ambaye ni Kinara wa Wachache hana ule uvumilivu wa kusikiza mawaidha yanayotofautiana na yake. Kwa Kiingereza inaitwa intolerance. Kila mmoja aliye kwenye Jumba hili alichaguliwa na alitumia mali yake, akili na hata muda wake kutafuta kura, kujitafutia na kutafutia mrengo wake wa kisiasa. Tusifike hapa watu waanze kuhujumu wenzao kwa sababu wengine wetu wameenda ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus