GET /api/v0.1/hansard/entries/1001115/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1001115,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1001115/?format=api",
"text_counter": 98,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Hata mimi nimesimama hapa kutaka kuongea na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchukuzi. Nafikiri Mhe. Abdullswamad Nassir aliuliza swali hili kwa sababu jambo hili limekuwa na utata mkubwa sana. Kama alivyosema Mwenyekiti, tuliweza kuwa na mkutano wa Wabunge kutoka Pwani, wakiongozwa na wa Mombasa, pamoja na Kamati ya Uchukuzi. Vile vile, pia, tukawa na mkutano pamoja na Rais, Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta, kwa swala hili. Kwa hakika, swala hili ni nyeti na ni swala ambalo limeharibu ajira nyingi sana ya watu wa Pwani na Wakenya kwa jumla. Wakati kulipotolewa ile tunasema kwa Kiingereza directive ya kusema ya kwamba zile shehena zote lazima ziende Naivasha, tulilizungumzia swala hili na kuambiwa ya kwamba maagizo kama haya ama hizi directives ziliweza kutolewa na ikawa ya kwamba kazi zitaendelea kama The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}