GET /api/v0.1/hansard/entries/1001116/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1001116,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1001116/?format=api",
"text_counter": 99,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "zilivyokuwa zikifanyika. Lakini, baada ya muda mfupi tu, tumekuja kuona kwamba swala lile limerudi vile vile. Tukiuliza tunaambiwa ya kwamba ni kwa sababu ya janga la COVID-19. Mhe. Naibu Spika, kweli tunajua COVID-19 iko nchini lakini swala lolote lingefaa watu waitwe mkutano ama wafanye ile tunasema kwa Kiingereza public participation na tuambiwe ya kwamba directives hizi zimerudi kwa sababu ya COVID-19, zimerudi kivipi, ni kwa muda gani na ikiwa zimerudi, je, tutaweza kufanya njia nyingine mbadala ambazo zinaweza kusaidia wakaazi wa Pwani na hata Wakenya kwa jumla? Kwa hakika, swala hili bado halijamalizika na majibu ambayo ameyatoa Mwenyekiti bado hayajakuwa na ufasaha na bado hawajalieleza jambo hili kwa undani. Kwa hivyo, bado tunataka Mhe. Waziri aweze kuweka kikao, kuja katika Bunge au kwa njia nyingine yoyote, kuweza kuzungumzia swala hili kwa sababu ni swala tata na nyeti na bado mpaka sasa kuna sitofahamu, hivi na hivi na hakuna mwelekeo. Asante Mhe. Naibu Spika."
}