GET /api/v0.1/hansard/entries/1002321/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1002321,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1002321/?format=api",
"text_counter": 143,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Hali ya uchumi na pesa kuzunguka katika uchumi wa Kenya vimefungiwa katika ofisi za ardhi. Vile vile, mawakili ambao wanafanya kazi zinazohusiana na Ofisi ya Ardhi, mimi nikiwa mmoja wao, wamefunga ofisi zao na biashara pia zimelala. Hii ni kwa sababu Ofisi ya Ardhi haifanyi kazi. Kazi zote za mawakili na wale wanaouza na kununua mashamba zimelala. Wengine wana shida na pengine wanatafuta namna ya kupata pesa za kwenda kutafuta matibabu nje ya nchi. Hali imekuwa ngumu."
}