GET /api/v0.1/hansard/entries/1003076/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1003076,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1003076/?format=api",
"text_counter": 160,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "Vijana hawakuwa wamelipwa siku nilipouliza hili Swali. Baada ya kuliuliza, vijana walilipwa. Nakubaliana na Mwenyekiti kuwa kuna vijana wamechukua mikopo ya Fuliza. Wengine wameweka majina ya girlfriends wao au waume wao. Hayo yametokea lakini tumefanya kikao na Assistant County Commissioner wa Mombasa na machifu. Tunajaribu kuyatatua kimjini. Hata hivyo, nina jambo kuhusu hili suala la vyombo na vifaa ambavyo walikuwa wapewe. Kwanza, kuna karatasi ambayo nimechukua kutoka Room 8 ama Table Office yetu ya Bunge. Ile karatasi inazungumza tofauti na alivyozungumza Mwenyekiti. Hii karatasi inaeleza wazi kuwa hawajatoa vifaa vyovyote. Ile Statement ambayo imesomwa na Mwenyekiti ni kuwa vifaa vimetolewa. Mimi mwenyewe kibinafsi natoa uhakikisho kuwa baadhi ya vyombo na vifaa vilivyotolewa kusaidia vilitolewa na Serikali ya kaunti, vingine vilitolewa na shirika la KeNHA, vingine vilitolewa na mashirika yasiyo ya kiserikali na vingine vilitolewa na kampuni zilizo katika sehemu ile. Naomba kwa unyenyekevu, hatupingi wala kufanya jambo lolote kinyume, tuone ni sawa kufanya kazi kwa pamoja ili tujue linaloendelea. Kwa hivyo, ingekuwa bora Mwenyekiti aulize suala hili la hivi vyombo ambavyo vinasemekana vimechukuliwa ili visije vikawa vimechukuliwa vikapatiwa vijana walio katika mjini na vijana walio mashinani hawajaviona vifaa hivi. Asante."
}