GET /api/v0.1/hansard/entries/1003515/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1003515,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1003515/?format=api",
    "text_counter": 133,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Zawadi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13176,
        "legal_name": "Christine Zawadi Gona",
        "slug": "christine-zawadi-gona"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Naunga mkono wenzangu kwa yale wanayo jadili kwamba tumekosa haki na imani kwa polisi. Pia, sio polisi wote kama vile wenzangu wanavyo zungumza, lakini ukweli ni kwamba nidhamu imekosekana. Kuna utepetevu fulani katika Idara ya Polisi ambayo imefanya wengi wetu kukosa imani nao. Juzi nikiwa naelekea nyumbani, nilipofika Kilifi kabla sijaingia nyumbani, jioni kama Saa Mbili hivi iki karibia Saa Tatu, nilimkuta polisi akimfukuza mtu. Huyo mtu alipita mbele ya gari niliyokuwa, ikasimamishwa gafla na nikashuka. Mwajua kuwa tuko na sheria inayosema kwamba watu wawe nyumbani Saa Tatu inapofika. Nilimsimamisha huyo polisi nikamuliza: “Kwa nini unamfukuza huyu mtu?” Akasema: “Tunamfukuza kwa sababu Saa Tatu imekaribia na bado yuko njiani.” Nikawauliza: “Vile mumemfukuza, kama angegongwa na gari, ni vipi ungekuwa umemsaidia na hiyo sheria? Ni kwa nini mumfukuze mtu? Kwa nini msipeane fahamisho ili watu waelewe? Watu wanajua hii sheria na kama mtu amekosea na anakimbia, anajua kwamba amekosea. Anakimbia ili afike nyumbani kabla Saa Tatu haijampata njiani. Hata hivyo, bado polisi wana chukua sheria mikononi mwao na wanafanya vile wanataka."
}