GET /api/v0.1/hansard/entries/1003516/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1003516,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1003516/?format=api",
    "text_counter": 134,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Zawadi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13176,
        "legal_name": "Christine Zawadi Gona",
        "slug": "christine-zawadi-gona"
    },
    "content": "Bw. Spika, kule Kilifi kuna bahari. Kuna msemo usemao “Nishike samaki kumi, nishike samaki mmoja, harufu yangu ni ile ile ya samaki.” Hatutasema harufu yangu ime shika samaki mmoja au kumi! Itakuwa harufu ni ile ile. Kwa hivyo polisi wawe wazuri au wawe vipi, lakini tumekosa imani nao, Idara yao ime oza na kuna utepetevu wa nidhamu! Kuchukuliwe haki kutoka kwao kwa sababu akiuawa mmoja na jami, utaona polisi wote wametoka kupiga watu wa hiyo mtaa mzima, hakutakalika eti askari mmoja alipigwa. Lakini wana ua watu wetu kila siku na hakuna kitu kina fanyika. Ni mmoja katika askari mia moja utaona sheria imechukuliwa dhidhi yake lakini wengi wana potelea. Mwingine anapewa transfer anapelekwa mahali pengine. Ni makosa! Bw. Spika, namaliza kwa kusema, ukishika samaki mmoja au samaki kumi, harufu ni ile ile! Naomba polisi wawe na nidhamu. Asante."
}