GET /api/v0.1/hansard/entries/1003653/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1003653,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1003653/?format=api",
"text_counter": 76,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bi. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Arifa iliyoulizwa na Seneta wa Taita/Taveta kuhusiana na pesa zinazotolewa kwa maswala ya kupambana na ugonjwa wa Korona. Bi. Naibu Spika, wiki mbili zilizopita, tulibahatika pamoja na Kamati ya COVID- 19 kusafiri Kaunti ya Isiolo kwa minajili ya kuona jinsi wamejitayarisha kupambana na janga hili. Jambo la kusikitisha ni kwamba hata Ofisi ya Gavana ilikuwa haina nafasi ya kuweza kutu pokea kama Maseneta ambao tulikuwa huko hususani kuanaglia ile miradi ya kaunti kuhusiana na maswala ya Korona. Bi. Naibu Spika, tulipelekwa katika police pavilion ambayo ndugu yetu Sen. Linturi alikuwa akitembelea zamani wakati alipokuwa kijana akijivinjari. Hapo ndipo tuliwekwa kunzungumzia maswala muhimu ya Korona. Huo ni mfano wa kaunti moja tuu ambayo tulizuru kama Kamati. Inamaanisha kwamba mambo mengi ambayo tunaona katika vyombo vya habari kwamba vifaa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}