GET /api/v0.1/hansard/entries/1003656/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1003656,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1003656/?format=api",
    "text_counter": 79,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bi. Naibu Spika, ufujaji wa pesa ni jambo ambalo liko wazi. Jana maafisa wa Kenya Medical Practitioners, Pharmacists and Dentists Union (KMPDU) walikuwa wanalalamika ya kwamba kaunti tano hazijalipa mishahara ya madaktari pamoja na wahudumu wa afya wakati huu tunapambambana na Korona. Ni vipi tutaweza kupambana na Korona ikiwa wafanyikazi hawalipwi mishahara? Daktari anafanya kazi katika hali ambayo ni ngumu. Anajihatarisha maisha yake na ya familia yake. Kwa mfano, anapewa barakoa moja. Hiyo ndiyo anaenda nayo nyumbani jioni. Kesho asubuhi anapewa ya pili. Bi. Naibu Spika, hili ni swala ambalo Kamati hii inaweze kuchunguza kwa undani na kuhakikisha pesa hazifujwi. Tukisubiri mpaka baada ya miaka miwili, tuje tusome reporti za CPAIC, itakuwa na hasara kwa Wakenya."
}