GET /api/v0.1/hansard/entries/1003836/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1003836,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1003836/?format=api",
"text_counter": 259,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa iliyoletwa Bungeni na Sen. Sakaja, Seneta wa Nairobi. Bi. Spika wa Muda, Serikali yetu imekuwa ikivunja sheria kwa sababu kila hati miliki ya ardhi inatolewa kulingana na sheria. Kwa hivyo, haiwezi kupokonywa yule mmiliki bila kufuata sheria. Wakati Waziri anatoa taarifa katika vyombo vya Habari kwamba atavunja ama kuweka ua katika nyumba za watu ambao wana hati zao, ina maana kwamba Serikali inasababisha kupuuzwa ama kuvunjwa kwa sheria, na hilo ni swala ambalo hatungeweza kulikubali kama Bunge, kuendelea kufanyika. Kila mtu anafaa apewe fursa ya kutetea ile hati ameweza kuipokea vipi? Je, ni vipi aliruhusiwa kujenga? Kuna shirika kama The National Environment Management Authority (NEMA) ambayo inafaa kuzingatia kabla ya kujenga. Unazingatia masharti unayopewa na NEMA ambayo inatakikana kujua kuwa hapa ni mahali pa msitu ama maji kupita na watu hawaruhusiwi kujenga. Bi. Spika wa Muda, kama ilivyotanguliwa kusemwa, wengi walijenga pale kwa sababu wamekuwa na matumaini kwamba itakuwa makaazi yao ya siku za usoni. Iwapo watavunjiwa hivi sasa, ina maana kwamba watu wale watashindwa kumiliki makaazi na watakuwa ni watu ambao wamerejea nyuma kimaisha kwa muda mmrefu. Katiba yetu inatoa haki ya kupewa malazi ama nyumba na Serikali. Mpaka sasa, haijaweza kuzingatiwa na kutekelezwa. Ikiwa Serikali inapokonya watu makao na ardhi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}