GET /api/v0.1/hansard/entries/1005386/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1005386,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1005386/?format=api",
"text_counter": 322,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Tumezungumziwa mambo ya Nandi, Migori, Kakamega, ambako kuna madini lakini watu wetu hawafaidiki. Hivi majuzi Kaunti ya Turkana kulipatikana mafuta ya petroli lakini rasilimali hiyo haiwafaidi Waturkana na Wakenya wote kwa jumla. Kule kwetu Pwani, rasilimali kubwa tuliyopewa na Mungu ni bahari. Watu wengi wanajikimu kimaisha kutokana na bahari. Bandari ya Mombasa haijafaidi Wapwani kisawasawa tulivyotarajia. Hivi majuzi, tulileta Arifa hapa Bungeni kulalamikia utendakazi inayohamisha bandari kutoka Pwani kuipeleka kule Naivasha. Hili ni swala linahusiana na rasilimali za maeneo ambazo mpaka sasa hazifaidi wale ambao wanakaa maeneo yale."
}