GET /api/v0.1/hansard/entries/1005392/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1005392,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1005392/?format=api",
"text_counter": 328,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Arifa hii ni muhimu sana kwa sababu inagusia sehemu zote za nchi hata maeneo ambayo haina rasilimali za madini. Kuna rasilimali za aina mingi kama; mifugo au wanyama pori ambazo zinaweza kusaidia kuinua hali ya uchumi wa wananchi pamoja na kaunti ambazo zinahusika. Kamati husika lazima iangalie swala hili kwa undani Zaidi ili kuhakikisha kwamba haturejei hapa tena kuzungumzia swala hili ambalo limekuwa donda sugu kabla ya uhuru wa nchi hii. Kabla ya kupata Uhuru, tulikuwa tunapigania rasilimali. Waliokuwa katika maeneo ya White Highlands, walikuwa wanapigania mashamba ambayo ni rasilimali yao. Wapwani tulikuwa tunapigania uchumi wetu ili tuweze kuimarika na kuinuka. Ni jambo la kusikitisha kwamba sasa, karibu miaka 60 ya Uhuru, bado tunaendelea kulalamika wakati tuna Katiba ambayo inaweza kutusaidia sisi kuhakikisha kwamba dhulma kama hizi za kihistoria zimewekwa kikomo na wananchi kupata faida ya mali na rasilimali ambazo ziko katika maeneo yao."
}