GET /api/v0.1/hansard/entries/1005730/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1005730,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1005730/?format=api",
"text_counter": 207,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13200,
"legal_name": "Issa Juma Boy",
"slug": "issa-juma-boy"
},
"content": "Kamati hi maalum, Sen. Malalah; Naibu Mwenyekiti, Sen. Halake, na wanakamati wengine waliochunguza swala hili. Nakubaliana na Maseneta wenzangu kwamba Maseneta waliohudumu katika Kamati hi ni watu wenye busara sana wakiwemo Sen. Madzayo. Kama Sen. (Prof.) Kamar alivyonena, namhimiza Seneta wa Kaunti ya Kirinyaga kuhakikisha kwamba Gavana na wawakilishi wa bunge la Kaunti ya Kirinyaga wanapatanishwa ili kutatua shida zinazowakumba. Sio Kaunti ya Kirinyaga tu ambapo gavana haelewani na wawakilishi wa bunge la kaunti. Tatizo hili linakumba kaunti nyingi humu nchini. Hatuombi kwamba hoja kama hili iletwe hapa Seneti tena lakini shida inaweza kuwa ni wawakilishi wa bunge la kaunti au gavana. Nashukuru Kamati ya Seneti iliyoangazia swala hili kwani ilifikia uamuzi wa busara sana. Kamati hiyo iliangazia kila mashtaka moja kwa moja na kuona kwamba kila kitu kiko sawa. Siku nyingine kukitokea tatizo kama hili, kamati itakayochaguliwa iweze kufanya kazi nzuri kama Kamati hii iliyoangazia swali hili. Bw. Spika, naunga mkono ripoti ya Kamati Maalum."
}