GET /api/v0.1/hansard/entries/1005735/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1005735,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1005735/?format=api",
    "text_counter": 212,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Naipongeza Kamati Maalum iliyoongozwa na naibu mkuu wa wachache katika Bunge la Seneti, Mhe. Malalah na naibu mwenyekiti wake, Sen. Halake. Nawapongeza Maseneta wengine pia waliohudumu katika kamati ile wakiwemo, Sen. Madzayo, Sen. Mugo, Sen. Mwangi na wengineo wote walioendesha kazi ile kwa tajiriba kubwa kabisa. Kamati ile ilijitolea na kuhakikisha kwamba imekamilisha ripoti yake kwa muda uliowekwa. Nampongeza Gavana Waiguru kwa kujitetea mbele ya Kamati. Pia, tuliona umuhimu wa familia katika maswala kama haya. Wakili Kamotho Waiganjo alichukua mambo mikononi mwake ili kuhakikisha kwamba ndoa yake haiwezi kusambaratika kwa kumtetea mke wake, Gavana Waiguru, asing’atuliwe mamlaka ya ugavana."
}