GET /api/v0.1/hansard/entries/1005922/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1005922,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1005922/?format=api",
    "text_counter": 161,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale CWR, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Zuleikha Hassan",
    "speaker": {
        "id": 13130,
        "legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
        "slug": "zuleikha-juma-hassan"
    },
    "content": " Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi kuchangia Hoja hii. Naunga mkono Ripoti ya Kamati ya Bajeti na Makadirio. Licha ya changamoto zilizotajwa na Wabunge wenzangu, nafurahi sana kwa sababu wafanyakazi katika sekta ya afya nchini wamepewa fedha za kununua vifaa vya kujikinga kutokana na maradhi ya Korona. Vile vile, wameongezewa marupurupu kuwasaidia kupigana na changamoto za kibinafsi zinazowakumba kwa sababu ya kupigana na ugonjwa huu wa Korona. Nimejua zaidi na nimeleta Hoja tofauti Bungeni kuhusiana na masuala ya afya na Wakenya wa kawaida wanavyoteseka kwa kuwa sekta hii ya afya haiendeshwi vizuri katika kaunti tofauti. Nasikitika kusema kuwa, hivi majuzi, kakangu ambaye ni daktari katika hospitali Kuu ya Pwani alishikwa na ugonjwa wa Korona. Aliugua na nashukuru alipona na hakuhitaji kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi. Hivi sasa, anasubiri kupimwa tena kuhakikisha kuwa hana ugonjwa huo. Ni muhimu kuangalia masuala ya wafanyikazi wa afya nchini kwa sababu wanaumia pamoja na familia zao kwa kutuhudumia sisi Wakenya wengine na kuhakikisha kuwa maradhi haya hayasambai kote nchini. Nimefurahishwa na Rais kutoa mgao huo."
}