GET /api/v0.1/hansard/entries/1005923/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1005923,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1005923/?format=api",
"text_counter": 162,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kwale CWR, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Zuleikha Hassan",
"speaker": {
"id": 13130,
"legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
"slug": "zuleikha-juma-hassan"
},
"content": "Ningependa kusisitiza Kamati ya Afya hapa Bungeni na kule Seneti kuhakikisha kuwa hizi fedha zinafika kule zilikolengwa na ziziharibiwe vile zimekuwa zikiharibiwa. Kama muda utaniruhusu, nataka kumuunga mkono dadangu, Mhe. Gladwell kutoka Baringo, alivyosema kuwa mara nyingi Serikalini tunazungumzia shilingi bilioni moja kama pesa kidogo sana. Nafahamu kuwa Mheshimiwa Ichung’wah alijaribu kumrekebisha. Nataka kukubaliana na Mhe. Gladwel kuwa kwa Mkenya wa kawaida, kwa shilingi bilioni moja, akitoa shilingi elfu moja kila siku, atatumia hiyo pesa kwa miaka 2,739. Kwa hivyo, ni pesa nyingi. Naomba tujizatiti kama Bunge kuhakikisha kuwa hizi fedha zinafika kule zinakostahili. Ahsante."
}