GET /api/v0.1/hansard/entries/1006015/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1006015,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1006015/?format=api",
    "text_counter": 68,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mvita, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika. Kupitia Kanuni za Kudumu Nambari 44(2)(c), naomba kuuliza na kusisitiza tena kupitia Kamati ya Uchukuzi, Kazi za Umma na Nyumba kuhusu ulazimishaji wa kusafirisha mizigo kupitia reli maarufu Standard Gauge Railway (SGR). Tarehe 2 Juni, 2020, nilileta ombi hili kuhusu ulazimishaji wa kusafirisha mizigo kutumia SGR. Ilipofika tarehe 16 Juni, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchukuzi, Kazi za Umma na Nyumba akaleta Ripoti ambayo inatofauti kubwa na vile hali ilivyo mashinani. Alisema huu ni mpangilio wa Marais wa nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki ya tarehe 12 May, 2020. Alisema kwamba mizigo yote ya nchi za nje lazima itumie reli kwa sababu ya kuzuia mripuko na mchipuko wa maradhi ya Korona. Jawabu lake likaendelea kusema kwamba Mawaziri wa nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki wamepatiwa amri kutekeleza agizo hilo. Ripoti ambazo ziko zinaonyesha kuwa nchi ya Uganda imekataa ulazimishaji wa kutumia reli. Pili, gharama alizozitaja Waziri za usafirishaji wa mizigo hazilingani na zinatofauti kubwa mno na zile wahusika wanazolipa na kutumia. Tatu, Waziri anasema kutumia SGR ni jambo ambalo nchi zote zimekubaliana kuwa litazuia uenezaji wa Korona. Nchi jirani ya Uganda imekataa jambo hilo. Nne, kusema kuwa Naivasha Inland Container Depot (ICD) iko tayari inaenda kinyume na ripoti ambayo iliwekwa sahihi na nchi ya Uganda, Rwanda na Sudan Kusini ya tarehe 22 May. Hakuna utafiti wowote ambao umefanywa wa athari ya kiuchumi kwa watu wetu wa Mombasa na wanaofanya kazi na kuishi kwa njia ya reli. Bw. Spika, kupitia hayo, ningeomba uweze kutoa amri kwa Kamati husika walete ripoti ya undani na ukamilifu ikizingatia yafuatayo – (i) Ni sababu ipi imemlazimisha Waziri kutoa amri hii bila ya idhini ya Bunge wala ufuataji wa sheria? (ii) Tukisubiri ripoti hiyo, kutolewe amri kwamba Bunge lisimamishe agizo hili mara moja mpaka watu waweze kuwasiliana, na hususan waliohadhirika. (iii) Ripoti hiyo ieleze kinagaubaga adhari za hali ya kiuchumi ya watu wa Mombasa na wale wengine wanaoishi na kufanya kazi katika njia ambayo mizigo hii hupitia, ikiwa mpangilio huu utaendelea. Ahsante, Bw. Spika. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}