GET /api/v0.1/hansard/entries/1006020/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1006020,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1006020/?format=api",
    "text_counter": 73,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mwita, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
    "speaker": null,
    "content": " Bw. Spika, ikiwa Mwenyekiti ameomba muda wa mwezi mmoja, basi ni sawa. Hatuwezi kukaa na watu wanaendelea kuwa walala hoi na huku inaonekana kana kwamba Bunge halifanyi kazi yake. Tukianza kuzungumzia muda wa mwezi mmoja ni sawa. Kabla ya ripoti ya Kamati, Waziri muhusika anapaswa kutoa amri ya kuwa agizo alilotoa ambalo halina kanuni yoyote ya kisheria, lisitekelezwe kwa sasa. Tungelipinga, lingelikuwa limeletwa hapa Bungeni. Ili kuonyesha kwamba Serikali iko na nia nzuri na watu wa Mombasa na wale walioko kwenye maeneo mengine yaliyoadhirika, agizo hilo liwekwe kando mara moja. Baada ya kuliweka kando, ripoti ya Kamati inapowasilishwa hapa, kila mmoja atakuwa amehusika. Wenye kuzungumza kwenye vibaraza ambao hawaleti malalamishi Bungeni na wale wenye kuzungumza Bungeni, wote waweze kuleta maoni yao. Lakini, kuanzia sasa hadi wakati huo, ninaomba kwa unyenyekevu tuweze kuelewana kwa sababu nchi nzima inatuangalia kama Bunge. La sivyo, wiki ijayo, kabla ya Bunge kwenda mapumzikoni, aweze kutueleza mahali ambapo Kamati imefika ili tujue hali halisi ilivyo."
}