GET /api/v0.1/hansard/entries/1006185/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1006185,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1006185/?format=api",
"text_counter": 238,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": " Mhe. Spika, katika Jumba hili, kama kuna watu ambao wanajulikana kwa hekima zao, wewe ni mmoja wao na utaingia kwenye kumbukumbu za historia kwa sababu ya hekima ambayo umeweza kuitumia hususa hivi sasa. Mmeweza kueleza lugha ya kisheria. Ningetaka tuzungumze lugha ya mtaani. Mpuuzi mpe sifa. Baadaya yote yale, hili Jumba ni Jumba ambalo rekodi zote zinawekwa. Inajulikana wazi ni nani anayeleta masuala yakutetea watu zaidi ya yeyote mwingine. Historia ipo katika Hansard iliyo hapa. Inajulikana wazi ni nani. Lakini leo, nakumbuka maneno ya marehemu Mzee wangu akiniambia usihofie…Nakumbuka kauli ya kuwa pale unapoona ya kuwa ghafla, mawe yanaanza kutupwa kwa kiwewe… Ile lugha yakunikashifu mimi, familia yangu mpaka marehemu baba yangu aliyoko chini kwenye kaburi kwa sababu ya kauli za jana, nawaambia tu kama vile ulivyozungumza wewe, Bwana Spika, namsamehe. Leo, kuna Wabunge watakaopoteza viti vyao kwa sababu Mahakama imewahukumu. Ikiwa kuna jambo lolote ambalo Abdullswamad Sheriff Nassir, kama Mjumbe wa Mvita, alikeuka na kuchukua kandarasi yoyote ya haramu, basi naomba afuate njia mwafaka ili jina langu litolewe kuwa sifai kuwa kiongozi. Hivi si vita vya sasa. Vita vinapangwa kwa sababu ya mwaka wa 2022. Lakini Jumba hili halidanganyi. Inajulikana wazi tetesi za mambo ya Poti ni nani aliyozungumzia tangu mambo ya CT2 Privatisation . Ina julikana ni nani alipitisha Mswada huo. Hili Jumba halidanganyi. Inajulikana ni nani aliyehakikisha kuwa Waziri aliregea nyuma kauli yake ya kwanza kuhusu mambo ya Standard Gauge Railway (SGR). Hili Jumba halidanganyi kuhusu yale yote tuliwafanyia wafanyi kazi wa Poti. Inajulikana wazi ni nani aliyewatetea. Siku zote hizo nilikuwa sijapewa kandarasi. Lakini mnasema nimepewa kandarasi kwa sababu sitaki kukubaliana na mambo ambayo ni ya upotofu wa sheria na naona wazi kuwa njia unayokwenda wewe ni njia ya kutanga tanga kisiasa. Nitaendelea kuhudumia watu wangu wale wale. Naomba kwa unyenyekevu, kuwa uwaambie wengine ambao unaketi nao katika lile gumzo la baraza kuwa mazungumzo yote pale yasife. Wayachukue wayapeleke katika Mahakama. Hiyo ndiyo njia mwafaka na kisa sawa cha kusema kuwa Abdullswamad Sheriff Nassir hafai. Historia na rekodi inaonyesha wazi msimamo wangu uko vipi. Leo wengine wanasema ni kwa sababu ya Baba ndio nakataa. Siku zote nilipokuwa ninapinga mbona sikuambiwa kuwa Baba alinikataza? Vile wamemtaja maheremu baba yangu, nitamalizia na kauli yake. Wapende wasipende tutaifanyakazi hii vile inavyotakikana."
}