GET /api/v0.1/hansard/entries/1006975/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1006975,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1006975/?format=api",
    "text_counter": 467,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kapenguria, JP",
    "speaker_title": "Hon. Samuel Moroto",
    "speaker": {
        "id": 318,
        "legal_name": "Samuel Chumel Moroto",
        "slug": "samuel-moroto"
    },
    "content": "Vile tuko na ugatuzi, Mswada huu utasaidia uongozi wa kaunti. Najua ya kwamba itasukuma na kuelekeza matakwa ya wananchi pale mashinani ili waanze kufaidika. Kama vile mmoja wetu alisema, kuna eneo ambalo jamii mbalimbali wanaishi kama Kapenguria. Wanaifanya sehemu hiyo kuwa cosmopolitan . Ni sehemu ambayo kila aina ya jamii inapatikana. Wakati wa kampeni, ukijihusisha na jamii fulani, watu wengine watakunyima kura. Hali hiyo huchangia kuwatenganisha Wakenya wanaoisha katika sehemu kama hizo. Kuna mahali watu wawili walikuwa wanang’ang’ania kiti cha ugavana. Yule aliyetangulia kwa uchaguzi huo alikua amekamilisha kipindi chake cha kwanza na mwingini akawa anampinga kwenye uchaguzi. Ikawa huyu mwingine anajaribu kuwaangamiza kabisa wale watu waliotangulia katika kipindi hicho kilichopita. Kwa hivyo, naamini kwamba Mswada huu ukipitishwa na uanze kutumika, utawaleta watu pamoja. Kila mmoja ambaye amepewa jukumu atajua kuwa atakuwa akifanya kazi akifuata sheria. Siyo kwamba atafanya vile anavyotaka."
}