GET /api/v0.1/hansard/entries/1007067/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1007067,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1007067/?format=api",
"text_counter": 41,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundayi, WDM-K",
"speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
"speaker": null,
"content": " Asante Mheshimiwa Spika. Naomba msamaha kwa kuchelewa kidogo. Mheshimiwa Spika nauliza Swali kwa Waziri wa Utalii na Huduma za Wanyama wa Pori. (i) Je, Waziri amepata ripoti kuhusu tumbili wanaosababisha hasara kubwa na uharibifu katika Eneo Bunge la Wundanyi? (ii) Ni hatua gani Wizara inachukua kukomesha mgogoro kati ya watu na wanyama na hasa kudhibiti idadi ya tumbili walio Eneo Bunge la Wundanyi ambao wanasababisha hasara kubwa na uharibifu wa mimea hivyo kuathiri vibaya kipato muhimu cha watu wa eneo bunge langu? (iii) Je, ni mipango gani Wizara inafanya kuwalipa fidia wakulima ambao wametiwa hasara ya mimea na vyakula vyao kuharibiwa na wanyama hawa? Asante Mhe. Spika."
}