GET /api/v0.1/hansard/entries/1007132/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1007132,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1007132/?format=api",
    "text_counter": 106,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Wundanyi, WDM – K",
    "speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
    "speaker": {
        "id": 13509,
        "legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
        "slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
    },
    "content": " Asante, Mhe. Spika. Ningependa kumpongeza mwenzangu, Mbunge wa Lang’ata kwa haraka alioichukulia suala hili na watu wake wakampa malalamishi yao na kuleta Bungeni. Mawaziri wetu wamekuwa wakisimama mikutanoni na kutoa maneno makali ambayo hayafuatilii miundo misingi ya kisheria. Hivi sasa tunapambana na janga la Korona, lakini Waziri alisema kuwa atawafungulia wanyama pori wavamie wananchi ambao hawana hatia. Leo hii, watoto wanaogopa Korona lakini katika eneo Bunge la Mhe. Korir, watoto sasa wanaogopa tena wanyama pori. Maneno ya Waziri ambayo hayapimwi yameleta uoga mahali pale. Ni vyema Waziri anapotamka jambo, awe amelichunguza kwa makini na sio tu kutia watu uoga. Mhe. Korir na wale ambao tunakaa maeneo yale tunaulizwa na wananchi tunafanya nini kuhusiana na suala hili. Ninajua baadhi ya wananchi wanaotoka kwenye eneo bunge langu ambao wamechukua mikopo, wengine mwaka jana tu. Hivi sasa, wanalipia mikopo, mamilioni ya pesa na inashangaza sana Waziri anapotangaza ya kuwa watu wanaoishi pale wana hatia. Ni vizuri iwapo Bunge hili litawafanya Mawaziri kuwajibika wanapotamka mambo yasiyo na misingi wa kisheria. Ninaunga Mkono ombi hili. Mhe. Spika, kabla niketi… The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}