GET /api/v0.1/hansard/entries/1008201/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1008201,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1008201/?format=api",
    "text_counter": 159,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mvita, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika. Nitatumia lugha ya taifa, Kiswahili. Wiki iliyopita, tulikubaliana na ukatoa amri kuwa Kamati ya Uchukuzi iweze kukaa na tukaweza kukaa jana na tukaafikiana vile mwenzangu alivyozungumza kwa Kiingereza kuwa amri ya kusafirishwa kwa mizigo na makasha yanayopelekwa nchi jirani kutumia SGR, kama ilivyokuwa amri ya kwanza ya kupeleka mizigo mpaka Nairobi, haipo tena. Wameiondoa amri hiyo. Huu si ushindi wa upizani bali ni ushindi wa hekima ya kutumia sheria vile inavyotakikana. Pili, kwa sababu Bunge hili hutengeza miswada na sheria, nawaomba Wakurugenzi wa Shirika la Reli nchini, wale wa Halmashauri ya Bandari ya Kenya, na wale wa Halmashauri ya Kukusanya Ushuru (KRA) wasitafute sababu ya kuwa hawakuambiwa. Bunge lina nguvu kuwaliko. Nina imani kuwa wale wenye kutufahamu wataelewa kuwa hawataki vita na sisi. Kwa hivyo, amri hii iweze kutekelezwa bila kusubiri na bila jambo lolote. Mwishowe, tumekubaliana na mwenzangu na tutarejea majumbani na kuzungumza na washikadau wote ambao ni mawakili, wafanyabiashara na wenye kuhusika na mambo ya bandari. Mwisho na muhimu zaidi, tunauliza ni kwa namna gani SGR itawafaa watu wa Mombasa na Wapwani kwa jumla, na sio Wapwani na watu wa Mombasa waifae SGR. Pili, pia tutaenda sambamba kuhusiana na mambo ya bandari ya kuwa ni njia gani bandari yetu itatufaa sisi na kuwafaa wengine, na sio sisi kuifaa bandari. Ahsante sana, Mhe. Spika. Leo ni wazi kuwa Bunge limeonyesha kuwa lina hamu ya wananchi wa Kenya katika masuala haya."
}