GET /api/v0.1/hansard/entries/1008368/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1008368,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1008368/?format=api",
    "text_counter": 326,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taveta, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Mataifa. Si siri kwamba Kenya inalinda masilahi na imepeana makao kwa wakimbizi wa kutoka maeneo ya nchi jirani, haswa wale ambao wamekuwa na matatizo nyumbani kwao kwenye walikotoka na wakahamia huku kwetu. Walivyohamia hapa kwetu, Umoja wa Mataifa umekuwa ukishikana na Serikali yetu ili kuhakikisha kuwa wakimbizi hawa wanaweza kuishi kwenye maeneo yale bila hali ya wasiwasi. Lakini ni vizuri kuwa sheria hii ikishapitishwa itaweza kuwalinda wakimbizi hawa. Lakini juu ya hapo, wale ambao wamewapokea kwenye maeneo yao waweze kuishi vizuri na wao kama majirani na kujua baada ya miaka hii yote, hao wamekuwa ndugu zetu. Vilevile ni vizuri kufahamu ya kwamba kule ambako wakimbizi hawa wamekimbilia ni maeneo ambayo yana ukame mgumu. Hata wale ambao wanaishi kama majirani ambao wamewapokea katika maeneo yao pia wanastahili kutambuliwa na Umoja wa Mataifa. Yangu ni kuunga mkono na kushukuru kuwa Serikali yetu kwa miaka hii yote imekuwa ikiwalinda wakimbizi wa nje. Vilevile, tunajua kuwa watoto ambao wamezaliwa hapa nchini Kenya wanatakikana kuwa na haki kama watoto wetu. Wakimbizi wengine wamekaa hapa miaka zaidi ya 20 au 30 na wamejua kuwa hapa kwetu Kenya ni kama kwao nyumbani. Mhe. Naibu Spika wa Muda, naunga mkono."
}