GET /api/v0.1/hansard/entries/1009069/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1009069,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1009069/?format=api",
"text_counter": 114,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bi. Naibu Spika, taarifa ya Sen. Kihika ni muhimu, hasa tukizingatia kwamba wale wanaofurushwa katika maeneo yao wanamoishi ni watu lala holela. Jamblo la kwanza na la fedheha ni kuona kume bomolewa kwa nyumba za watu. Jambo hili si haki hata kidogo. Katika Kaunti ya Kilifi watu wamewahi kutimuliwa kutoka mashamba ya ADC. Pia diwani wa huko amewahi kutiwa ndani kwa sababu alikuwa anatetea watu wake. Haya mashamba ya ADC yamekuwa kama kidonda sugu. Serikali imesema ile ardhi iliyoko Sabaki irejeshewe wananchi. Hata hivyo, tumewaona mabwanyenye amabao wamejitwalia ardhi na kuikatakata vipande vipande na kusema huko ni kwao. Tayari wako na stakhabadhi miliki mashamba hayo. Huo ni ukora mkubwa amabao unafanya Wakenya wengi kuhangaika. Tukiangalia katika maeneo mengine kama Mtwapa, hivi sasa watu wanavunjiwa nyumba zao. Tumewahi kuongea hayo hapa ndani. Watu wamekuja na makaratasi na kudai hiyo ni ardhi yao na hali si yao. Watu wameishi hapo zaidi ya miaka hamsini. Sasa hao wananchi wote ni Wakenya. Wataenda wapi? Mambo ya kufurusha wananchi bila heshima yakome katika Serikali hii. Kumekuwa na Serikali zaidi ya tatu---"
}