GET /api/v0.1/hansard/entries/1011358/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1011358,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1011358/?format=api",
    "text_counter": 364,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "Cha kusikitisha ni kwamba ikiwa kuna kampuni kubwa au mradi mkubwa katika sehemu, kwa mfano, Lamu Port South Sudan Ethiopia Transport corridor (LAPSSET), katika mambo ya bahari inafaa yajitolee kabla kuanza mradi, waweke kitengo cha kusimamia majanga ambacho kitakuwa kikisaidia majanga yakitokea. Lakini hakuna hata moja, ingawa ni rahisi kwao kufanya kitu kama hicho. Watu wanakufa wakati huo, wanapata shida ama wanakataa kwenda kwa bahari lakini kama kungekua na njia ya kuwasaidia, wangekuwa wanaendelea na maisha yao ya kawaida. Watu wanaenda baharini wanapotea na majanga ya kila aina yanatokea lakini kampuni kubwa kama hizo hazitusaidii. Mswada huu utasaidia sana."
}