GET /api/v0.1/hansard/entries/1011404/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1011404,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1011404/?format=api",
"text_counter": 21,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Nimesimama kuambatana na Kifungu Nambari 48(1) cha Kanuni za Kudumu za Bunge la Seneti kuomba Taarifa kutoka kwa Kamati ya Barabara na Uchukuzi kuhusu hali ya Barabara ya Nairobi- Mombasa hususan maeneo ya karibu na Dongo Kundu, mjini Mombasa. Kwenye Taarifa hiyo, Kamati inafaa kuangazia yafuatayo- (1) Kueleza sababu za sehemu ya Barabara ya Dongo Kundu iliyozinduliwa takriban mwaka mmoja na nusu uliopita kukarabatiwa mara kwa mara. (2) Kufafanua chanzo cha maporomoko ya udongo yaliyo shuhudiwa kwenye barabara hiyo zaidi ya mwezi mmoja uliyopita na kusababishwa kufungwa kwa sehemu za barabara hiyo, na pia kusababisha msongamano mkubwa wa magari na wasafiri wanaotumia Bandari ya Mombasa. (3) Kueleza iwapo wahandisi waliohusika na ujenzi wa barabara hiyo walifanya utafiti wa kutosha kuhusu mchanga uliopo katika maeneo hayo kabla ya ujenzi ili kuhakikisha ni salama kwa ujenzi wa barabara hiyo. (4) Kutaja hatua zinazochukuliwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Barabara Kuu, yani KeNHA, kudhibiti hali katika barabara hiyo na kuhakikisha madhara kama hayo hayatokei tena katika eneo hilo. (5) Kueleza dhamana ya barabara hiyo ni ya miaka mingapi na ni nani anayegharamia ukarabati unaondelea kwenye barabara hiyo kwa sasa. Barabara ya Dongo Kundu ni mojawapo ya barabara muhimu ambazo zinasaidia watu kuhamisha mizigo kutoka Bandari ya Mombasa na kupelekwa maeneo ya bara. Kwa hivyo, kuharibika mara kwa mara kwa barabara hiyo kunachangia pakubwa kupunguza hali ya uchumi na kuzuia biashara katika Mji wa Mombasa na maeneo jirani. Barabara hiyo ni kitengo muhimu katika uchukuzi wa Mji wa Mombasa."
}