GET /api/v0.1/hansard/entries/1011420/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1011420,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1011420/?format=api",
"text_counter": 37,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Ningependa kujiunga na wenzangu niseme Taarifa iliyoletwa na Seneta wa Mombasa, Sen. Faki, ni muhimu sana kwa uchumi wa taifa hili. Utaona ya kwamba wakati wowote Serikali ikifanya mipangilio ya kujenga barabara za pwani wanaangalia mabarabara ambayo inaenda maeneo ya utalii. Hawajali barabara zinazoenda sehemu ambazo watu wanaishi kwa wingi. Bw. Spika, ni aibu kubwa kwa Serikali kuona kwamba barabara ya Dongo-Kundu ambayo haijamaliza miaka miwili, tayari imeanza kuporomoka na kuwa na mashimo. Uporomokaji huu umetokana na kutokarabatiwa kwa hali ya ustadi wakati wa ujenzi. Maeneo ya Diani, South Coast na Mji wa Mombasa kumejaa watu wengi sana. Kwa hivyo, ni lazima kuwe na barabara nzuri na hali ya usalama kuimarishwa, hasa wakati wa kusafirisha shehena kutoka na kuingia Bandari."
}