GET /api/v0.1/hansard/entries/1011422/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1011422,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1011422/?format=api",
"text_counter": 39,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Tumeona ajali nyingi zikitokea katika barabara ya kutoka Mombasa kwenda Malindi. Barabara hiyo haijakarabatiwa kwa zaidi ya miaka kumi. Hivi majuzi wanakandarasi walikuja hadi Mtwapa na kuanza kubomoa pande zote mbili za barabara kwa minajili ya kukarabati. Hata hivyo, hakuna barabara ambayo wanajenga bali ni kumwaga mchanga na seruji. Kitendo hiki kinasababisha ajali nyingi wakati magari yanabishana na kujaribu kukwepa mashimo na vilinduko vya mchanga na seruji. Barabara kama hizi zikiwa zinatengenezwa ni lazima watoe taarifa kuu katika mabango kuonyesha ni nani anayezijenga, ikiwa ni mkopo ni kutoka wapi na itachukua muda gani kukamilisha ujenzi. Barabara ambazo hunganisha maeneo mbalimbali ni lazima zikarabatiwe, haswa zile zinazoelekea kwenye maeneo ya wanaofanya biashara za kuuza mazao bidhaa ambazo zinaweza kuharibika kwa haraka kabla kufika Marikiti na masoko mengine. Ninaiomba Kamati itakayoangalia jambo hili izingatie maeneo ambayo watu wengi wanaishi. Kwa mfano, barabara hii ya Dongo-Kundu ni muhimu sana kwa wanabiashara ambao husafirisha mazao yao kutoka sehemu mbalimbali. Ninaiunga mkono Taarifa hii ya Sen. Faki."
}