GET /api/v0.1/hansard/entries/1012170/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1012170,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1012170/?format=api",
    "text_counter": 309,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Kwa sababu alikuwa karibu na yeye na alikuwa hamuangalii; alikuwa anaongea na Petronilla hapo. Bi Naibu Spika, ikiwa Rais mwenyewe wiki iloyopita alituambia tuweze kutafakari sisi kama Wakenya na akasema si lini shule zitafunguliwa bali ni kwa njia ipi. Jambo la kushangaza ni kwamba hata siku saba hazijapita kutokea Rais aongee msemo huo, tunamuona Waziri Magoha ametangaza kwamba watoto warudi shule. Hili ni jambo la kusikitisha kwa sababu hivi sasa Rais hajasema kwamba ugonjwa huu wa COVID-19 umeisha au katika Kenya si janga tena. Hatuwezi kucheza karata na maisha ya watoto wetu. This is very serious. Tutaanza kuona makaburi ya watoto wadogo yakitapakaa kila mahali nchini. Itakuwa jambo la aibu kuona ametoa amri kama hii, watoto wetu warudi shule na hatimaye tuanze kuzika vifaranga. Hili ni jambo la kutafakari na kufikiria zaidi. Jambo la pili, yeye akisema hivyo kwamba ameregesha, wakati huu tumempatia kutokea mwezi wa tatu, mpaka sasa tumefika mwezi wa kumi. Je, tujiulize ni matayarisho gani Wizara ya Elimu imefanya kuhusikana na hawa watoto wa darasa la nane ambao imesemekana warudi shule, kwa sababu wanatarajiwa kufanya mtihani mwezi wa tatu mwaka ujao? Kutarajia kufanya mtihani ni kama utafika na ugonjwa ukiwa umekupata je? Tunaambiwa wazi kabisa ya kwamba hawa watoto wadogo wakienda kucheza hawaangaliani vile wanacheza. Wanakumbatiana, wanacheza mpira na wanaongea. Hawana ile mambo tunayoita social distancing. Ni madawati gani yametengenezwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}