GET /api/v0.1/hansard/entries/1012205/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1012205,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1012205/?format=api",
    "text_counter": 344,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Asante sana, Bi. Naibu Spika. Nasimama kuunga mkono ripoti hii. Tumeona kwamba watabibu mara nyingi wanazembea kazini. Siku hizi mambo ya afya wanaangazia zaidi sana mambo ya fulusi. Wakati mwengine, inawezekana kwamba si watu wote ambao wana bima za afya na iwe bado idhini kutolewa kutumiwa wakati mtu amefika hospitalini. Hili swala halijawaadhiri tu wananchi wa kawaida. Hata hapa katika Bunge tumeona viongozi wakiwa ziara za nchi za kigeni wakikosa kupata huduma mwafaka kwa sababu hawawezi kugharimia matibabu wakizingizia kwamba idhini hazijapatikana. Juzi kulikuwa na kesi ya mama mmoja aliyepata mtoto nje ya Hopistali ya Pumwani bila kusaidiwa na wauguzi. Walipoulizwa kwa nini hawakumsaidia, walisema kwamba kazi yao si kazi ya bure au ya sulubu. Walisema ni lazima wapate haki zao. Katiba yetu inasema lazima mgonjwa apate matibabu ya dharura anapofikishwa hopitalini. Baadaye swala la pesa lishughulikiwa baadaye. Bi. Naibu Spika, swala hili halimhusu tu mama Virginia aliyeaga bali linahusu gharama ambayo watu wengi hupata katika hospitali nyingi za kibinafsi. Wakati mwengine wananchi wa kawaida huhitajika kununua dawa ambazo haziambatani na magonjwa yao. Ni swala zima la ubora wa afya katika nchi hii. Na tathmini ya kwamba sasa hivi afya inapatikana tu kwa wale walio na hela; maskini hana chake. Hatujui kama utakuwa na fedha leo na kesho hauna. Mwenyekiti wa Kamati, Sen. (Dr.) Mbito na aliyekua mwanakamati, Sen. Shiyonga, wamesema kuwa kazi yetu isiwe tuko na hii ripoti na mapendekezo yasiwe hayana mashiko yoyote. Tunafaa kuangalia swala zima la afya. Mtazamo huu pia unaangazia zaidi kwa sababu kama tungekuwa na hospitali za umma ambazo zinafanya kazi, basi hakungekua na biashara kubwa ambayo inaendelezwa na hospitali kama MP Shah. Ni kweli kuwa hospitali za kibinafsi zimeweka kukidhi akidi ambayo iko inayotokana na kutokuwa na huduma bora katika hospitali za umma. Hata ukiangazia mradi NHIF, bado utapata kuwa hospitali za kibinafsi zinafaidi. Napigia upato ripoti hii na ningemuomba Mwenyekiti, Sen. (Dr.) Mbito kwamba isiwe kama zingine. Ripoti hii inafaa kuwa kielelezo kwamba mwananchi yeyote ana haki ya kupata matibabu yanayofaa. Tutakuja kuzungumza mambo ya fedha baadaye ili tusipoteze maafa mengi. Maafa mengi yametokea lakini huyu ni Mkenya ambaye aliweza kufikia Sen. Mugo. Ni Wakenya wangapi ambao wanakufa na kunyanyaswa kutokana na kutokuwa na sauti au hawafiki wenzetu katika Bunge hili la Seneti? Naunga na kusema kuwa hii ripoti isisitizwe na iwe kielelezo katika nchi hii."
}