GET /api/v0.1/hansard/entries/1012212/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1012212,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1012212/?format=api",
    "text_counter": 351,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bi Naibu Spika, nami pia naunga mkono Ripoti hii ya Kamati ya Afya. Ni jambo la kusikitisha na aibu kwa Wakenya ikizingaitiwa kuwa mama alipoteza maisha yake. Kabla ya mtu kufuzu kuwa daktari, yeye huapa kuokoa maisha. Hospitali hiyo haikupewa leseni kufanya vitu kama hivyo. Waliapa kuokoa maisha ya binadamu kwa kuwapa matibabu. Hawafai kuweka pesa mbele kiasi ya kwamba mgonjwa anayekwenda kupata matibabu anakaa kwa muda mrefu akiangaliwa tu. Hatimaye maisha yake yanakatika muda unavyozidi kwenda. Hospitali hiyo imekiuka kiapo cha kuokoa maisha wanachokula madaktari. Huu ni mwaka wa 2020. Kuna maswali tunayofaa kujiuliza sisi kama Wakenya. Je, ni haki kuweka pesa mbele? Licha ya kuwa kuna hospitali za kibinafsi na za umma, je, tuna utu wa kuhudumia wagonjwa maskini au matajiri katika hospitali zetu? Unawezapata mtu ameumwa na nyoka na kupelekwa hospitalini bila pesa. Huenda akawa kwa maumivu na wakati huo sumu inaendelea kupanda. Hata hivyo, utapata kuwa mtu huyo anaangaliwa tu akigeuka rangi na hatimaye kupoteza maisha. Ni lazima tuzingatie mapendekezo ya Ripoti hii. Jambo la mwisho ni kuwa uzito unatokea wakati wa malipo ya madaktari, wahudumu wengine wa afya na wanaofanya kazi katika fuo za hospitali za umma. Kuna watu wanaofanya kazi bila vifaa. Kwa mfano, juzi tumeona wahudumu wakiandamana kwamba wapewe vifaa. Sasa hivi kuna janga la COVID-19 ilhali hawana mavazi ya kuwakinga. Hata kama mtu anafanya kazi ya kusafisha hospitali, ni lazima awe na vifaa vya kumkinga kutokana na ugonjwa. Serikali inafaa kutafakari haya. Ikiwa kuna watu wanaotakiwa kuangaliwa, ni wale wanaofanya kazi katika hospitali kwa sababu wanashughulikia maisha ya Wakenya. Ni jukumu la Serikali kuona kwamba hakuna migomo katika sekta ya afya Mara nyingi tunamwona Katibu wa Kudumu wa Chama cha Wahudumu wa Afya wa Kenya, Bw. Seth Panyako, akiteta kwa sababu ya malipo duni ya wahudumu wa afya. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}