GET /api/v0.1/hansard/entries/1012222/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1012222,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1012222/?format=api",
    "text_counter": 361,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bi. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa iliyoletwa Bungeni na Kamati ya Afya. Kwanza naunga mkono mapendekezo ya Kamati ya Afya kuhusiana na kifo cha mamai katika Hospitali ya M.P. Shah. Visa vya Wakenya kufariki katika hali kama hiii vinaendelea kuongezeka kutokana na ajizi ama utepetevu katika hospitali zetu na pia madaktari ambao viapo vyao hawawezi kuvitekeleza kikamilifu. Imekuwa ni biashara kubwa kufungua hospitali, lakini huduma zinazotolewa mara nyingi huwa haziridhishi. Ndugu yangu, Seneta wa Makueni, amezungumzia kifo cha Mwalimu Walibora ambaye alikuwa mwalimu wa Kiswahili mwenye tajiriba kubwa. Maisha yake ilimalizika katika chumba cha wagonjwa mahututi katika Hospitali kuu ya Kenyatta wakati waliposhindwa kumpa huduma muhimu ambayo alikuwa anahitaji ili kuokoa maisha yake. Wakati huu tukiwa tunazungumza katika Bunge hili, kuna wengine wanaopoteza maisha yao katika hali kama hii. Naipongeza Kamati ya Afya kwa kulishughulikia swala hili kwa muda mfupi na pia kutoa mapendekezo, kwamba iwapo hospitali nyingine itatokea kufanya utepetefu kama huu, kuna sehemu ambayo watu wanaweza kulalamika na malalamiko hayo yakachukuliwa kwa uzito, na haki kupatikana. Kama alivyotangulia kusema Seneta wa Makueni ni kwamba madaktari wanalindana katika taaluma yao kupitia chama chao cha KMPDU. Hawako tayari kumtoa kafara daktari mwenzao kwa jambo lolote linalotokana na utepetefu katika kazi yao. Wengi wanalindana na kuteteana. Hivyo basi, inakuwa ni vigumu kwa mhusika kuweza kudhibitisha mbele ya mahakama kwamba kifo kilitokana na utepetefu ama ajizi ya daktari yule. Bi. Naibu Spika, Ripoti hii ningependa ichukuliwe kwa uzito na Bunge hili, kuhakikisha kwamba mambo kama haya hayawezi kutokea tena katika nchi yetu. Shirika la NHIF linakataa kutoa malipo kwa wagonjwa wa ugonjwa wa COVID-19 ambao umezuka katikati ya mwaka. Kwa hivyo, hawawezi kupata bima ingine ambayo itawalinda na maswala kama haya. Hii Ripoti inafaa kutekelezwa kikamilifu ili tuhakikishe kwamba wale wanaofanya utepetefu katika kutoa huduma za afya na kusababisha vifo vya Wakenya hawaachwi kuwa huru nchini. Asante Bi. Naibu Spika."
}