GET /api/v0.1/hansard/entries/1012695/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1012695,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1012695/?format=api",
"text_counter": 374,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": " Ahsante Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii nichangie Hoja hii. Moja kwa moja, nataka kuipongeza Kamati kwa Ripoti yao nzuri. Lakini Kamati hii imeangazia sana upande wa Magharibi. Kwa hakika, sio upande wa Magharibi peke yake ambako miwa inapatikana. Miwa inaweza kupatikana kwa wingi upande wa Tana River na Lamu hata kushinda upande wa Magharibi. Kunaweza kutoka miwa nyingi eneo la mto Tana. Kilomita chache kutoka Mto Tana kunaweza toka miwa nzuri zaidi kushinda upande wa Magharibi. Utafiti uliofanywa unaonyesha kwamba miwa ya upande wa Magharibi inavunwa baada ya mwaka mmoja na nusu. Lau ingefanyika upande wa Tana River na Lamu, sana sana Lamu, miwa hiyo inawezavunwa baada ya miezi kumi. Utafiti tena ukaonyesha kwamba tunaweza kuzalisha miwa na kupata tani 100 kwa kila ekari moja. Upande wa Magharibi mwa Kenya, ekari moja huzalisha tani 80. Lamu inaweza kupatikana tani 360 kwa siku. Tunajua kwamba kila tunapokwenda tunaliliwa mambo ya kazi. Watu wanatafuta kazi. Hizi ndizo nafasi za kazi. Kamati hii ikitia akilini jambo hili, inafaa kufikiria kaunti nyingine pia; sio upande wa Magharibi peke yake. Sekta hii itatoa kazi nyingi. Pia tutakuwa tumechangia katika zile Agenda Nne za Rais. Tutakuwa na uzalishaji mwingi. Tunaweza mpaka kusafirisha. Na sisi Lamu tuna bandari ambayo iko karibu. Twaweza kuitumia ile bandari kwa faida ya Wakenya na wakazi wa Lamu pia. Tusingojee kutoa miwa au sukari kutoka huku. Twaweza pia kutumia bandari ya Lamu kusafirisha. Pia itakuwa ni faida kwa Serikali. Mhe. Naibu Spika wa Muda, ndio tunasema pesa zipelekwe mashinani ndio tuweze kuzalisha mashinani na watu watoke kwenye miji waende wakatafute kazi mashinani. Tukisema pesa ipelekwe tu kwenye watu wengi, basi tutasababisha kuwe na idadi kubwa ya watu katika miji. Naiomba Kamati hii au Bunge, tafadhali, lipitishe hii Ripoti au mtaandika nyingine na mhakikishe mmeiweka Lamu ndani ili tuweze kuzalisha sukari. Watoto wenu watakuja kufanya kazi kule. Haimaanishi mkipeleka pesa Lamu ni watu wa Lamu tu ndio watafaidi. Hapana! Bandari iko Lamu au Mombasa lakini wanaofanya kazi kule ni Wakenya wote. Narejelea: Pelekeni pesa mashinani ili tutoe watu kwenye miji waende wakafanye kazi mashinani. Mkiweka pesa huku, watu watajaa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}