GET /api/v0.1/hansard/entries/1012709/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1012709,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1012709/?format=api",
    "text_counter": 388,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Hata mimi pia ningependa nizungumzie suala hili la ukuzaji wa sukari. Kila sehemu katika Jamhuri ya Kenya iko na uti wa mgongo wa uchumi wake. Hakika kwa watu wa Magharibi na Nyanza, sukari imekuwa uti wa mgongo katika uchumi wao. Suala hili la sukari ni suala nyeti kwa sababu viwanda hivyo vya sukari vilikuwa vimeajiri zaidi ya watu 40,000. Pia, vilikuwa vinafaidisha watu zaidi ya laki moja ambao ni wakulima wa miwa na, hivyo basi, kuweza kufaidisha zaidi ya watu milioni mbili katika taifa letu la Kenya. Ni masikitiko makubwa ya kwamba viwanda hivi vyote vilikufa na hivyo basi tukapoteza ajira na maisha kwa Wakenya wenzetu. Hivi sasa, Rais wetu amezungumzia ajenda zake nne. Katika ajenda moja, amezungumzia mambo ya viwanda. Basi iwapo ako na ajenda kama hio, ni wazi kabisa Ripoti kama hii itekelezwe ili tufufue viwanda hivi. Tumeona ya kwamba changamoto nyingi zilikuwa katika sera. Kumekuwa na sera duni ambazo zimesumbua sana wakulima wetu kuendelea na kilimo kwa njia ilio sawa. Vile vile, kumekuwa na ushindani. Wakulima wetu hawana uwezo wa kushindana na wakulima kutoka nchi za nje katika biashara ya sukari. Vile vile, soko ilikuwa changamoto kwa sababu nchi yetu iligeuka ikawa ni sehemu ya kutupia sukari kutoka nchi za nje. Sukari ile inahujumu juhudi za wakulima wetu na kufanya sukari inayokuzwa na wakulima wetu kukosa soko hata hapa kwetu Kenya, mbali na zile nchi zingine za nje. Kwa hivyo, jambo kama hilo, kama tunataka kuenda mbele kama taifa la Kenya, lazima tulizingatie sana. Vile vile, tunafaa kujenga taaluma zaidi kwa wakulima wetu katika ukuzaji wa sukari. Hivi sasa, tuna lengo na madhumuni ya kufufua viwanda kama hivi. Hilo litakuwa suala muhimu sana. Vile, vile, lazima kuwe na fedha na hazina maalum kwa sababu hivi ni viwanda vilivyokuwa vizuri na vimeboresha maisha ya Wakenya na kuboresha uchumi wa taifa la Kenya. Hivyo basi, katika harakati za kuvifufua, lazima kuwe na hazina maalum ambayo itahakikisha ya kwamba Ripoti hii na yale ambayo sisi tumeyapendekeza yanatekelezwa bila taswishi yoyote. Suala lingine ni kuwa wafanyakazi walikosa mishahara. Swali ni: Je, mishahara ilikosekana kwa nini? Katika Ripoti, tunaona kuna ufisadi ambao ulikithiri kwa kiwango ambacho hata wakulima walishindwa kupata mapato yao. Hata wafanyakazi walishindwa kupata mishahara yao. Hayo yalihujumu ukuzaji wa miwa na kuhujumu viwanda vyetu vilivyokuwa wakati ule. Jambo lingine ambalo nataka kuzungumzia ni utekelezaji wa sheria. Yale ambayo kama Bunge la Taifa tumezungumzia lazima tuyachukulie kwa upeo wa juu sana. Tusiwe tu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}