GET /api/v0.1/hansard/entries/1012710/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1012710,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1012710/?format=api",
"text_counter": 389,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "tutazungumza kisha ripoti inawekwa kando bila utekelezaji. Sasa ni wakati wa Bunge kuhesabika katika kufufua ukuzaji wa viwanda vya sukari. Leo tunaona katika miji yetu watu wengi wamejaa; kumekuwa na msongamano kwa sababu kule nyanjani, kule mashambani, hakuna ajira yoyote wala viwanda vyovyote. Wakenya wote wanakimbilia mijini. Kwa hivyo, iwapo tunataka kukabiliana na mambo kama hayo, lazima kuwe na viwanda mashinani na viboreshwe kwa hali ya juu kwa tekinolojia."
}