GET /api/v0.1/hansard/entries/1013626/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1013626,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1013626/?format=api",
    "text_counter": 39,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Sana, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia ombi ambalo limeletwa Bungeni na Bw. Nashon Ogana. Kwanza namuunga Bw. Ogana na wenzake mkono kwa kuwa na imani kwamba Bunge la Seneti litasaidia kutatua ombi lao. Imani hiyo imesababishwa na kwamba sisi kama Maseneta tunayaangazia matatizo kama haya kwa njia ya haraka na kutoa suluhisho mapema kuliko taasisi zingine ambazo zimewekwa na sheria za kutatua malalamiko kama haya."
}