GET /api/v0.1/hansard/entries/1013627/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1013627,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1013627/?format=api",
"text_counter": 40,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Swala kama hili likipelekwa mahakamani, linaweza kuchukua zaidi ya miaka kumi kabla ya suluhisho kupatikana. Kamati husika litakalo angazia ombi hili ishughulike kwa haraka ili kuwe na suluhisho kwa muda mfupi iwezekanavyo. Hii ni kwa sababu mizozo ya mipaka kama hii husababisha watu kupoteza maisha, uharibifu wa mali, wizi wa mifugo na mali zingine za wananchi wa Kenya. Ni jambo la kuhuzunisha kuwa karibu miaka 60 ya Uhuru hatujaweza kutatua matatizo madogo kama ya mipaka ambayo yako kote nchini. Kuna mizozo ya mipaka kati ya Kaunti Makueni na Taita Taveta, Taita Taveta na Kwale, Taita Taveta na Kajiado, Kisumu na Vihiga, Kitui na Tana River, Garissa na Tana River na kati kaunti zingine. Mizozo ya mipaka imetapakaa kote nchini."
}