GET /api/v0.1/hansard/entries/1013902/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1013902,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1013902/?format=api",
    "text_counter": 29,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "hivi sasa, Serikali haijachukua hatua mwafaka kuweza kulipa wanakandarasi ama hawa wauzaji wa vitu vidogo vidogo katika shule zetu. Wanaosoma katika shule hizo ni watoto wetu wala sio wa watu wengine ama kutoka nchi zingine. Hata kama kuna watoto wa kutoka nchi zingine, hao ni wanafunzi wanaotaka kukimu mitihani, ili waweze kuendelea. Ikiwa tabia kama hii itaendelea, na wanakandarasi hawa wakose kupeleka vifaa hivyo shuleni, basi shule hizo pia zitakuwa hazina uwezo wa kufundisha wanafunzi. Tunaweza kufahamu ya kwamba, kabla hujakuwa mwanakandarasi, kwanza kwa sababu unapeleka vitu vidogo vidogo, unaenda na kuweka nyumba na cheti cha kumiliki ardhi kama rehani ili uweze kupewa mkopo. Mara nyingi mkopo huu huwa na muda. Usipolipa unaweza kupata nyumba yako ama shamba lako linauzwa, halafu inakuwa ghasia ama shida kubwa kwa familia. Hata inakuwa yule mzazi pengine anashindwa hata kupeleka watoto wake shuleni kwa sababu ya lile deni kubwa lililoko katika benki ambalo liweza kuongezeka riba. Hivi sasa tukiongea, ile kandarasi haiwezi kupeanwa, kwa sababu watu hawaelewi ni asilimia gani ambayo naweza kulipwa ili waweze kujipanga kusambaza vifaaa tena. Matatizo kama haya yasilete shida kwa wale wanakandarasi wanaopeleka vifaa katika shule zetu. La mwisho, kuna uzembe wa ufisadi ndani ya Wizara hii ya Elimu. Ikiwa hawawezi kulipa, je hizo pesa ambazo zimetengwa huwa zinaenda wapi? Ni lazima hawa wanakandarasi ama wauzaji wa hivi vitu vidogo vidogo ambavyo vinatakikana katika shule zetu walipwe mara moja wanaposambaza vifaa kwa shule hizi."
}