GET /api/v0.1/hansard/entries/1013916/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1013916,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1013916/?format=api",
"text_counter": 43,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika. Nataka kuunga hii Petition ya huyu ndugu yangu, Sen. Mwaruma, Seneta wa Taita-Taveta kuhusikana na hili shamba la Msambweni ambalo liko katika Voi Constituency, Kaunti ya Taita-Taveta. Bw. Spika, shamba hili liko katika kijiji cha Mkamenyi ambacho kiko katika Kaunti ya Taita-Taveta. Historia ya shamba hili ni ya kusikitisha. Ijapokuwa kulikuwa na wenyeji pale, walichukuliwa kama wanyama na shamba hili likachukuliwa na kupewa mzungu kwa sababu zisizoeleweka, lakini iliepeanwa kama zawadi. Wenyeji wanaoishi katika hilo shamba sio wanyama. Bw. Spika, ni jambo la kusikitisha kuona kwamba si mara ya kwanza, ya pili na haitakuwa ya mwisho kusema kuwa mashamba mengi katika eneo la Pwani yamepewa kwa watu binafsi kama zawadi ya kufurahisha mtu. Tulipopata uhuru, Rais wa Kwanza, Mzee Jomo Kenyatta, alipeana sehemu fulani kama zawadi kwa watu fulani ambao ni mabwenyenye katika ardhi iliyoko baharini na maeneo mbali mbali eneo la Pwani. Tunaona ya kwamba katika maeneo haya---"
}