GET /api/v0.1/hansard/entries/1013921/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1013921,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1013921/?format=api",
    "text_counter": 48,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bw. Spika, sijui kama ni kwa sababu ya sintofahamu za Sen. Sakaja na Sen. Kinyua kutamka maneno kama hayo. Taarifa hii. ambayo imesomwa na Sen. Mwaruma kutoka Taita Taveta inahusikana na mkoa wa Pwani. Sehemu ambayo imetajwa ni Msambweni na Kamheni ambayo iko Taita Taveta. Aliyepewa shamba ni askari jeshi wa kizungu ambaye ametajwa hapa na Sen. Mwaruma. Kuna Ripoti ya Truth, Justice and Reconciliation Commission (TJRC) ambayo ilitaja watu ambao walipewa ardhi ya Pwani. Kama Sen. Kinyua hajui, chanzo cha Lake Kenyatta anakijua. Tuliuliza tinga tinga, tukapewa watu. Kama hiyo si zawadi, sijui kama kuna zawadi nyingine tena. Ni jambo la kusikitisha mpaka hivi sasa tukiongea kuwa swala la Taita Taveta si shamba pekee, bali hata milima iliyoko Taita Taveta kuanzia Voi hadi Milimani ambapo watu wanatoa tanzanite, ruby na green granite ambayo ni rasilimali kama dhahabu, ina pesa nyingi zaidi."
}