GET /api/v0.1/hansard/entries/1014185/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1014185,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1014185/?format=api",
"text_counter": 76,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "kujua ni hesabu zipi ambazo ziliweza kutumika. Ni hekima ipi ama vigezo, almaarufu criteria, iliyoweza kutumika au ni sayansi ipi iliyoweza kutumika ikawa ni sehemu hizi mbili peke yake katika Kenya ndio zilizofaa kufungwa si mara moja bali kuendelea. Pili, ni muhimu kujua kutoka kwa Waziri ikiwa wameweza kufanya utafiti kujua hali ya kijamii na kiuchumi, baada ya athari za kufungwa. Serikali ina nia gani kuhusiana na wakazi wa Old Town na Eastleigh kuongeza mapato yao ya kiuchumi baada ya athari hii ya kufungiwa? Mwishowe, tunaomba waziri aongeze rasilimali hususa katika maeneo athirika kupitia mfuko wa kukabiliana na dharura ambao kwa Kiingereza unajulikana kama Emergency ResponseFund ili wakazi wetu waweze kusaidika. Ni rahisi sana kwa yeyote kuleta fujo na ghasia ikiwa hali ni mbovu, lakini hekima ni pale unapoyatatua matatizo ya watu wako hali ikiwa imetulia. Tulikuwa tunaogopa kwanza kuuliza maswala pale mbeleni serikali isije ikasema sasa munauliza ndio tunafunga zaidi. Sasa, maadam tunaona wazi kuwa hesabu zinapungua, ni sawa wale wakazi wa Old Town na Eastleigh waweze kujua hatima yao na ilikuwaje haya yote yakafanyika. Pili, Serikali ihakikishe uchumi wao umeongezeka ikiangaliwa ya kuwa huko Old Town na Eastleigh kihistoria imejulikana kuwa ni mahali ambapo watu wanaenda kufanya ununuzi wa bidhaa zao, kwa Kiingereza shopping. Ahsante sana, Mhe. Spika."
}